Mrithi wa ufalme nchini Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman ndiye aliinunua nyumba ya kifahari nchini Ufaransa kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la New York Times.
Gazeti hilo linasema kuwa ununuzi huo wa mwaka 2015 ulifanywa kuputia kampuni kadhaa za shell.
Nyumba hiyo iliyo karibu na Versailles ina sehemu nyingi za kifahari ikiwemo sinema.
Iligharimu dola milioni 320 na jarida na Fortune likaitaja kuwa nyumba ghali zaidi duniani.
Mnunuzi hakujulikana wakati huo.
Lakini New York Times inaripoti kuwa nyaraka zilionyesha kuwa nyumba hiyo ilimilikiwa na kampuni inayosimamiwa na wakfu wa Prince Mohammed.
Serikali ya Saudi Arabia haijasema lolote kuhusu ripoti hiyo.
Mwaka 2015 Prince Mojammed aliripotiwa kujinunulia mashua ya kifahari kutoka kwa mfanyabiashara raia wa Urusi kwa dola milioni 590.
Post a Comment