Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuanza kuifanyia marekebisho katiba na kufuta kifungu cha kuwepo au uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Abdulghafar Idrisa(aliyesimama)
Msimamo huo
ulitangazwa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Abdulghafar Idrisa Juma
wakati alipozungumza katika hafla ya kuyapokea matembezi ya Vijana 400 wa
UVCCM waliotembea kwa miguu
ili kuadhimisha miaka 53 ya mapinduzi ya zanzibar .
Abdulghafar
amesema kimsingi na kimantiki hakuna katiba yoyote duniani
inayoandikwa kwamba Taifa hilo litaunda Serikali ya Umoja wa
Kitaifa, shiriki au kuwa na Serikali ya mpito.
Ameeleza kuwa aina
ya muundo wa serikali hizo hutegemea na hali halisi na mazingira
kulingana na matokeo ya uchaguzi mkuu au matokeo ya kura na viti vya kila chama
kilivyoshinda.
Amebainisha kuwa
Serikali ya Chama cha Mapinduzi toka awali ilikuwa na nia njema ya kutaka iwepo
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini si kwa kuandikwa katika katiba ya
nchi kama ilivyotokea kwa katiba ya zanzibar.mawaziri
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.