0





Timu ya Liwale B fc iliyovaa jezi nyekundu ndivyo hapa ndipo walianza vurugu na kuamua kushikilia mpira mkononi 
Leo ikiwa juni 24 katika Ligi ya Liwale Super Cup kulikuwa na mchezo mmoja kati ya timu ya Hawili fc dhidi ya Liwale B fc mchezo uliochezwa uwanmja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika mchezo wa leo timu ya Hawili fc iliweza kushinda bao 3 bila magoli yote matatu yakifungwa na Ramadhani Hashimu namo dakika ya 48,53 na bao la mwisho dakika ya 72. 

Namo dakika ya 85 ya mchezo timu ya  wachezaji wa Liwale B fc walianzisha vurugu na kuamua kukaa nao mpira na kugomea kuendelea na mchezo na kuamua kutoka nje ya uwanja.

Kocha wa timu ya Hawili fc aliweza kuangea na Liwale Blog alisema timu yake imecheza vizuri lakini ameitupia lawama timu ya Liwale B fc kutoka uwanjani kabla ya mpira kumalizika.

Kaimu katibu wa ligi  Abdala Kipaga alisema kwa mujibu wa kanuni ya ligi hii endapo timu ikianzisha vurugu itakuwa imejitoa katika kuendelea na mashindano haya.

Post a Comment

 
Top