Watendaji
na watumishi katika taasisi za Serikali wameaswa kutokutumia mali ya umma kwa
maslahi yao binafsi.
Afisa idara ya utawala bora ofisi ya
Raisi katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora Zanzibar, Hassan Vuai
ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika mafunzo ya siku mbili kuhusu haki
za binadamu na utawala bora yaliyoandaliwa na kituo cha huduma za sheria
Zanzibar katika ukumbi wa kituo hicho Kijwangani mjini Unguja.
Amesema kufanya kazi kwa uaminifu,
uadilifu na huruma inajenga misingi ya maadili katika utawala bora ambapo
amesisitiza watendaji pamoja na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuwajibika katika
majukumu yao ya kila siku ili kuchochea utawala bora nchini.
Pamoja na hayo afisa hayo amezitaja
athari zinazosababishwa na ukiukwaji wa misingi ya maadili katika utekelezaji wa utawala bora kuwa ni
pamoja na uwepo wa huduma duni hasa za kijamii, rasilimali za nchi kunufaisha
wachache na taasisi za umma kufanya kazi bila ufanisi.
Post a Comment