0


Simba sc imeendelea kuweka recod nzuri ya kuwafunga wapinzani wao yanga kila wanapokutana katika Ardhi ya Zanzibar baada ya kuwafunga kwa tofauti ya penalti 4-2 katika mchezo wa nusu fainali ya mapinduzi Cup uliopigwa hapo jana majira ya 2:30 usiku katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar

Hatua hiyo ya mikwaju ya penalti imekuja mara baada ya timu hizo kutoshana nguvu ya bila kufungana katika kipindi cha dakika tisini za mchezo huo ulioudhuriwa na mamia ya mashabiki kutoka maeneo mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania bara.
Penalti za Simba zilifungwa na Nahodha Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Muzamil Yassin na beki Mkongo Janvier Besala Bokungu, wakati kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa beki Mzimbabwe Method Mwanjali.
Waliofunga penati za Yanga ni Simon Msuva na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wakati kipa Mghana wa Simba, Daniel Agyei aliokoa penalti za Dida na Mwinyi Hajji Mngwali.
Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kulitia majaribu lango la Simba dakika ya kumi, baada ya Nahodha wake Haruna Niyonzima, kupiga shuti akiwa nje ya 18 lililodakwa na kipa Mghana Daniel Agyei.
Yanga tena wakalisakama  lango la Simba dakika ya 15, baada ya winga Simon Msuva kupiga mpira uliorudi kufuatia pigo la mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe kuokolewa, lakini kipa Agyei akaokoa tena akishirikiana na beki Method Mwanjali.
Simba wakajibu dakika ya 16 baada ya kiungo Mohammed Ibrahim kupiga shuti kali lililodakwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi.
Msuva  akakaribia kufunga dakika ya 35 baada ya kumtoka kwa chenga nzuri beki wa kulia wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kumlamba chenga ya mpira wa kichwa kipa Agyei, lakini akapigwa  pigo dhaifu lililokuwa linaelekea golini na  beki Janvier Besala  Bokungu akatokea na kuokoa.
Kwa ujumla timu zote zilishambuliana kwa zamu, lakini Yanga ndiyo waliomiliki mpira zaidi wakicheza kwenye eneo lao na kuvusha upande wa pili hivyo kuwafanya viungo wa Simba muda mwingi wawe na kazi kubwa kutafuta mipira  katikati ya Uwanja.

Kipindi cha pili, Yanga walikianza vizuri pia na kufanikiwa kupata kona dakia 47, ambayo hata hivyo ilipigwa ovyo na Niyonzima na kuokolewa kwa urahisi.
Dakika ya 47 Mo Ibrahim akipiga shuti kali  lililodakwa na Dida na dakika ya 54, Simba wakapiga kona mbili mfululizo, lakini hazikuzaa matunda
Kwa ujumla Simba na Yanga zimekutana mara nne hadi sasa kwenye ardhi ya Zanzibar na Yanga imeshinda mara moja mwaka 1975 kwenye fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mabao 2-0 ya Sunday Manara na Gibson Sembuli (marehemu).

Mechi nyingine zote Yanga wamefungwa na mbali na hiyo ya 2011 ya Mapinduzi, walifungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1, Simba wakitangulia kwa bao la Hussein Marsha na wao kusawazisha kwa bao la Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu) na Nusu Fainali ya Ligi ya Muungano 1-0, bao pekee la Damian Kimti zote mwaka 1992.
Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo, ikitoka kufungwa 4-0 na Azam FC katika mechi ya mwisho ya Kundi A Jumamosi, wakati Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys Jumapili.

Simba sasa itakutana na Azam FC Ijumaa katika Fainali. Azam imeitoa Taifa Jang’ombe katika mchezo uliotangulia jioni ya jana na Azam akafanikiwa kupata ushindi bao 1-0.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, MOhammed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk72, James Kotei, Juma Luizio/Pastory Athanas dk77, Muzamil Yassin na Mohamed Ibrahim/Laudit Mavugo dk85.
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke/Emmanuel Martin dk63.

Post a Comment

 
Top