Mwanamume mmoja
nchini Uganda amezikwa pamoja na dola 5,700 pesa taslim, ambazo alitaka
kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake na kumuokoa kutoka kwa
moto wa ahera.
Charles Obong, mfanyakazi wa zamani wa serikali
ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 52, aliomba hilo kwenye wosia
wake, kwa mujibu wa familia yake.
Licha hiyo kutekelezwa, kaburi
lake lilifukuliwa na pesa hizo kuondolewa kutoka wa jeneza lake, baada
ya wazee wa jamii kufahamu kilichotokea, kwa mujibu wa gazeti la the
Daily Monitor.
Gazeti hilo lilimnukuu askofu mmoja wa kiangilikana
Joel Agel, akisema hakuna pesa zinazoweza kununu uzima wa milele na
Mungu hawezia kupokea pesa kama malipo.
Post a Comment