Mahakama nchini
Marekani imemuhukumu adhabu ya kifo mzungu mwenye msimamo mkali, ambaye
aliwaua waumini tisa weusi katika kanisa moja, Carolina ya Kusini.
Dylann Roof alikutwa na hatia mwezi uliopita kwa zaidi ya mashtaka 30, ikiwemo uhalifu wa chuki.
Katika maelezo yake ya mwisho kwa mahakama hakuonesha kujutia makosa yake na kusema bado anahisi alipaswa kufanya mauaji hayo.
Mwezi
Juni 2015, alikwenda katika kanisa moja la watu wenyea asili ya Afrika
mjini Charleston na kufyatua risasi wakati somo la dini likiendelea.
Kesi
hiyo ilizua mjadala mkubwa kuhusiana na masuala ya ubaguzi wa rangi
nchini Marekani na kumlazimu Rais Barack Obama kutaka kumalizwa kwa
ghasia zinazosababishwa na matumizi ya bunduki.
Post a Comment