Rais Barack Obama
ametoa hotuba yake ya mwisho kwa taifa muda mfupi uliopita katika jimbo
la Chicago, ambapo sehemu kubwa ya hotuba yake imejikita katika
kuainisha mafanikio yake katika kipindi chake cha urais.
Rais
Obama amesikika akisema, ilipoanzia ndipo itakapoishia. Akiwa na maana
kwamba Chicago ndipo alipoanzia siasa zake akiwa pamoja na Michelle
Obama, na alipata ushindi mkubwa sana katika mji huo. Kwa hiyo, ni eneo
ambapo lina historia muhimu katika maisha yake ya kisiasa lakini pia ni
kama njia moja wapo ya kusema asante kwa wana Chicago.
Hotuba hii ina tofauti kubwa sana na zile nyengine, hii ikiwa ni hotuba ya mwisho ya Obama kama rais wa Marekani.
Hotuba hii imeangazia mambo mbali mbali ikiwemo kuwataka wamarekani wawe na umoja.
Rais
Obama pia ametumia muda wake mwingi sana kuzungumzia demokrasia na
kusema kwamba katika kipimo cha demokrasia watu wanaweza kuanguka kwa
pamoja au kuinuka kwa pamoja.
Kuhusu mahusiano ya kimataifa,
amezungumzia jinsi alivyoweza kutatua mgogoro wa Iran na mradi wake wa
nuklia, lakini pia ameweza kuhuisha tena uhusiana wa Marekani na Cuba.
Post a Comment