Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
amesaini rasmi muswada wa moja ya kipengele cha katiba ya Zanzibar
baada ya kufanyiwa marekibisho na baraza la wawakilishi katika kikao
kilichopita.
Uthibitisho
huo ameutoa Ikulu hapa Zanzibar wakati akiongea na waandishi wa habari
wakati wa mazungumzo yake kuhusu muswada wa mafuta ambapo amesema
ameuridhia muswada huo kwa vile kipengele hicho kinachohusu uteuzi wa
nafasi mbili za wawakilishi za upinzani zisingeweza kwa rais kuteua
kutokana na sheria hiyo ambapo nafasi hizo zilikuwa zikiteuliwa kwa
kushirikiana na kiongozi wa upinzani lakini hakijaeleza endapo hakuna
upinzani ndani ya baraza rais atateua vipi ilihitaji marekebisho.
Na
katika hatua nyengine vyama viwili vikubwa vya siasa Zanzibar chama
tawala CCM na chama kikuu cha upinzani CUF vimetoa maoni yao kuhusu
muswada wa mafuta ulisainiwa na kuwa sheria na rais wa Zanzibar Ikulu
juzi ambapo wakati CCM kupitia kwa naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar
Vuai Ali Vuai imempongeza Dkt. Shein kwa vile ametekeleza ilani ya
uchaguzi ya CCM na ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni, kwa CUF katibu
mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharrif Hamad ameuita muswada huo ni
batili kwa vile hata hautaji mipaka ya Zanzibar na kinyume na katiba ya
Jamhuri ya Muungano na hakuna sheria ikapitishwa ikawa juu ya katiba
ambapo bunge lilipaswa kubadilisha kipengele cha katiba kuhusu suala la
mafuta kutokuwa la muungano.
Miswada
hiyo miwili yote ilijadilaiwa ndani ya baraza la wawakilishi katika
kikao kilichopita na miswada hiyo ilijadiliwa na kuchangiwa na wajumbe
wote wa baraza hilo ambapo wote walitoka katika chama cha Mapinduzi na
wajumbe watatu kutoka chama cha ADA-TADEA, AFP na ADC.