0
Obama and Duterte

Rais wa Marekani Barack Obama amekutana kwa muda mfupi na mwenzake wa Ufilipino, Rodrigo Duterte nchini Laos baada ya mkutano wa awali kufutiliwa mbali.
Mkutano wa sasa umefanyika siku chache baada ya kiongozi huyo wa Ufilipino kuonekana kumtusi Obama kwa kumuita "mwana wa kahaba".
Maafisa wamesema mkutano huo umefanyika kabla ya dhifa ya jioni wakati wa mkutano wa viongozi wa eneo la Kusini Mashariki mwa Asia ambao umekuwa ukifanyika mjini Vientiane, mji mkuu wa Laos.
Mzozo ulianza pale Bw Obama aliposema angemuuliza kiongozi huyo maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya Ufilipino.
Lakini Bw Duterte, ambaye ameunga mkono mauaji hayo, alisema iwapo hilo lingefanyika: "Putang ina (mwana wa kahaba) nitakutusi katika mkutano huo."
Alisema nchi yake kwa sasa haitawaliwi na taifa lolote.
Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani zamani.
Baada ya matamshi yake kuzua utata, Bw Duterte aliomba radhi na kusema hakukusudia kumshambulia kiongozi huyo wa Marekani.
  Wachanganuzi wanasema tabia ya Duterte inamfanya kupendwa sana nyumbani lakini huenda akatengwa na jamii ya kimataifa
Wachanganuzi wanasema tabia ya Duterte inamfanya kupendwa sana nyumbani lakini huenda akatengwa na jamii ya kimataifa
Alieleza matumaini kwamba wanadiplomasia wa Marekani na Ufilipino wangetatua mgogoro huo.
Tangu kuingia madarakani, Bw Duterte ameendelea kutumia maneno makali, na kutumia lugha chafu kuwarejelea Papa Francis, maafisa kadha wa Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na balozi wa Marekani nchini Ufilipino.

Post a Comment

 
Top