0

 
 NB-Siyo picha ya mtu huyo wa ajabu
Wakazi wa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wameingiwa na hofu baada ya mtu asiyejulikana kudaiwa kuwaingilia kimwili kimazingara “kufanya mapenzi kimiujiza” katika nyumba zao nyakati za usiku na kuiba mali.


Wakiongea na mwandishi wa Malunde blog ,Steve Kanyeph wanakijiji hao wamesema mtu huyo huingia katika nyumba za watu usiku wa manane bila wao kutambua na kisha kuwaibia hasa simu zao za mikononi,taa aina ya sola,sabuni na kuwaingilia kimwili wanawake bila waume zao kujua.


Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na Malunde1 blog kwa masharti ya kutotajwa majina yao wanasimulia kisa hiki….


“Unakuta umelala na mume wako cha kushangaza unamkuta mwanaume wako kalala chini au nje ya nyumba … mtu huyo anakufanyia mchezo mchafu..lakini pia wakati mwingine milango na madirisha inakuwa imefungwa lakini ukiamka unakuta ipo wazi hakuna sehemu iliyobomolewa na simu zimeibiwa kama sio ushirikina nini jamani?”.

“Tayari ameingilia watu katika kaya tano na tunashindwa kuelewa huyu mtu wa namna gani,wengine hawafanyishi mapenzi bali akikuta kuna pesa anachukua kidogo na kkuacha zingine”,anasimulia mhanga wa tukio hilo.

“Huyo mtu ana miguu miwili mmoja wa binadamu mwingine wa punda,huwa anapuliza dawa mlango unafunguka saa nane usiku,huyu mtu hajulikani ni wa aina gani”,ameongeza shuhuda mwingine wa tukio hilo.



Mwanamke mwingine aliyekumbwa na kadhia ya mtu huyo alisema aliingiliwa usiku wa saa nane akiwa amelala ambapo alishtushwa na mtikisiko wa kitanda na kuhisi kuna tetemeko linapita hata hivyo alipojifunua shuka aliona mtu akimmulika kwa mwanga wa simu ya kiganjani akielekea kitandani kwake.


"Kwa kweli sielewi jinsi gani aliingia ndani, maana hata alipofika kitandani sikujua alivyofika na kuondoa chandarua, ghafla alitoweka, na nilipojikagua nilijiona na hali isiyokuwa ya kawaida",aliongeza.

Kamanda wa jeshi la jadi (sungusungu) kanda ya Nsalala, Nassoro Malaja alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa sasa wanaendelea na ulinzi madhubuti na msako mkali kwa ajili ya kumbaini na kumkamata mtuhumiwa huyo.
 

Mwenyekiti wa kijiji hicho Seni Shija amekiri kupokea taarifa hizo na tayari serikali ya kijiji imekaa kikao ili kutafuta utatuzi, pia amewaomba wananchi hao kuacha kuamini katika nguvu za giza kwani huo ni usumbufu wa vibaka tu.  Chanzo:Malunde1 blog

Post a Comment

 
Top