Tume ya haki za
binadamu nchini zimbabwe imesema kuwa watu wanaounga mkono upinzani,
walio kwenye maeneo yenye ukame wamenyimwa misaada ya chakula na chama
tawala cha ZANU-PF.
Mwenyekiti wa bodi maalum Elasto Mugwadi,
amesema kuwa kwa sasa uchunguzi umebainisha kuwa watu wanaounga mkono
upande wa upinzani wanaambiwa waziwazi kuwa hawatopewa msaada wowote wa
chakula na inaarifiwa kuwa watu wengi wameathirika kutokana na hali
hiyo.Taarifa ya serikali inaonyesha kuwa nusu ya wakazi wa vijijini
wamekumbwa na njaa, jambo linalochochea kupingwa kwa utawala wa rais
Mugabe.
Wakati huo huo mahakama kuu nchini humo imebatilisha
marufuku ya maandamano yaliyokatazwa na polisi kwenye mji mkuu wa
Harare. Ambapo marufuku hiyo ilidumu kwa muda wa wiki mbili.
Wanaharakati
wanne wanaopinga utawala wa rais Mugabe ndiyo waliwashilisha pingamizi
mahakamani kupinga uamuzi wa polisi kupiga marufuku maandamano kwenye
mji mkuu wa Harare.
Hakimu wa mahakama kuu ya nchini humo amesema
kuwa marufuku hiyo ya polisi ilikuwa batili. Siku za hivi karibuni
kumekuewa na ongezeko la wimbi la maandamano nchini Zimbabwe,
wakiandamana kuhusu mdororo wa uchumi nchini humo.
Maandamano makubwa yanaratibiwa na wanaharakati kupitia mitandao ya kijamii.
Post a Comment