0


Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), inatarajiwa kuingia nchini kesho ikitokea Canada.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana.


Itule alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.


“Ndege ya pili inatarajiwa kukabidhiwa Septemba 22 na kuanza safari ya kuja Tanzania Septemba 23,’’ alibainisha.

Post a Comment

 
Top