0
                        Tokeo la picha la love
Neno ‘I Love You’ au Nakupenda, si neno geni msikioni mwa wengi na huwa haliishi utamu na hamu.
                                   Tokeo la picha la love
Unaweza mwambia hivyo mpenzi wako, mara kwa mara, lakini umeshawahi kujiuliza maneno mengine mbadala ya kumwambia mpenzi wako ili mapenzi yenu yazidi kuwa mazito.

Yapo mambo mengi ya kumwambia mpenzi wako apate amani, hii inajenga upendo na Heshima kati yenu.

Mwambie Anaweza:
Kuna wakati tunapitia mambo magumu sana katika maisha na watu wanakata tamaa ya maisha wanakosa uthubutu wa kujaribu tena na tena, kama amefeli mtihani,amepata ajari ya gari, amepata hasara ya kibiashara mwambie “baby you can” mwambie anaweza kuendelea na maisha yataendeleea mtie moyo hii itamfanya ajiamini na kuona thamani yake kwako.

Unanivutia
Mwambie ni kiasi gani anakuvutia, mwambie alivyo mrembo/mtanashati mueleze ni kihasi gani unakuwa na furaha akiwa karibu nawe, hii itamsaidia mpenzi wako kujiamini. Msifie mpenzi wako kwa suti au tai yake mpya , msifie msichana kwa kiatu chake na gauni lake zuri kabla hajatoka nyumbani sababu anaweza akasifiwa na wengine kwahiyo kuwa wa kwanza kumpa sifa hizo atajisikia wa fahari.

Unajivunia kuwa Nae
Mambo yanaweza yasiwe vile mnavyotaka wakati wote, kuwa karibu na mwenza wako na umuelezee ni kwa kiasi gani unajivunia kuwa nae, nafasi yake katika maisha yako na umuhimu wake ni faraja kwako, mueleze na umuonyeshe pia matendo yanaongea zaidi ya maneno. Mwambie “am proud of you”

Omba Kutoka Nae.
“Let’s go out” hapa wasichana wengi huwa wanasubiri watoke na wapenzi wao mpaka waambiwe au mpaka mpenzi wake apange kutoka nae, chukua nafasi ya kumtoa mpenzi wako mara moja moja na ugharamie huduma zote za siku hiyo, kama ni safari ufukweni, hotelini au migahawa mjini.

Msamaha
Uwe mwepesi wa kusema neno samahani kila mara, kuna kukoseana mara kwa mara kuwa wa kwanza kuomba msahama hii itapunguza hasira za mapenzi wako na malumbano pia hayatapata nafasi, hii itasaidia kuhimarisha mahusiano ya muda mrefu.

Rafiki usisahau kumuita mpezi wako kwa majina mazuri na yenye kusisimua muite 'Honey', 'Darling', 'Sweety', 'Baby', Mahabubah, La 'Azizi, 'My Filigisi', 'My Everything', na mengine kadhaa yenye mfano huu.

Post a Comment

 
Top