0

 Dubai

Ndege ya Shirika la  Ndege la Emirates iliyokuwa ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Dubai imewaka moto  na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo.
 Ndege hiyo Boeing 777-300 ilikuwa na abiria 282 na wafanyakazi 18 na hakuna aliyejeruhiwa. Abiria wote waliokolewa kupitia mlango wa dharura wa ndege hiyo iliyouwa ikiruka kutoka Trivandrum, India.

 Waliondolewa kwenye eneo la tukio ndani ya dakika 45 tangu kwa ndege hiyo kuwaka moto huku vyombo vya zimamoto zikichukua hatua ya haraka kuudhibiti moto huo.
Ndege hiyo iliwaka moto muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja huo na kwamba hadi sasa hakuna taarifa za kile kilichobabisha kuzuka kwa moto huo.

Miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na 24 Wabritons, sita Wamarekani, wanne Waireland na wawili Waustralia

Post a Comment

 
Top