Moto
mkubwa ulizuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa leo.
Moto huo inasemekana ulisababishwa na uchomaji mashamba yaliyopo jirani
na uwanja huo. Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuzima moto huo ambao
ungeweza kuteketeza vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na majengo.
Akizungumza
katika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela
(pichani na fulana nyekundu) ambaye alishirikiana na kikosi cha zimamoto
kuzima moto huo alisema lazima wananchi wajue kutenga mashamba yao na
kuzuia mioto kusambaa
"Kuanzia
sasa yoyote atakaye sababisha moto kutoka kwenye shamba lake
atachukuliwa hatua kali za kisheria", alisema Mhe. Kasesela.
Mkuu
wa wilaya huyo piaaliagiza manispaa itengeneze kwa kutumia bullodozer
barabara ya kuzuia moto kuzunguka uwanja. Moto huo ulianza majira ya saa
7 mchana na kusambaa hadi kwenye uwanja wa kuondokea ndege (Runway) na
kusogelea eneo la kuhifadhia mafuta ya ndege na vifaa vya kuongozea
ndege. Ulidhibitiwa na Jeshi la Zimamoto vizuri na hadi kufikia saa 9.43
moto ulikuwa umezimwa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiliongoza gari la kuzima moto kuelekea eneo la tukio la moto katika Uwanja wa ndege wa Nduli, Mkoani Iringa.
Post a Comment