Polisi wa kukabiliana na ghasia walitumiwa kuwatawanya waandamanaji
Mmoja wa walioshuhudia anasema polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji.
Upinzani umevilaumu vikosi vya usalama kwa kutumia risasi dhidi ya maandamano yanayotaka kutangwazwe tarehe ya uchaguzi wa urais.
Upinzani umeitisha maandamano zaidi leo Jumanne.
Waandamanaji walifunga barabara na kuteketeza magari
Waziri wa mambo ya ndani Evariste Boshab amesema mmoja wa maafisa hao wa polisi aliuawa kwa kuchomwa moto akiwa bado yu hai.
Kuna wasiwasi kuwa rais Joseph Kabila ana njama ya kutaka kusalia madarakani baada ya kumalizika kwa muhula wake mwishoni mwa mwaka huu.
Mwandishi wa BBC aliyeko Kinshasa Poly Muzalia anasema polisi waliwakamata zaidi ya waandamanaji 10.
Upinzani waandamana dhidi ya rais Kabila DRC
Maandamano dhidi ya rais Kabila: Watu 17 wafariki DRC
Shule nyingi na biashara katika mji huo mkuu zilifungwa.
Kwa mujibu wa katiba, muhula wa pili wa Rais Kabila, aliyeingia madarakani baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka 2001, unafaa kumalizika tarehe 20 Desemba.
Mwaka uliopita, watu 12 waliuawa katika maandamao sawa na hayo.
Tangu kujinyakulia uhuru zaidi ya miaka 55, hakuna kiongozi aliyewahi kumkabidhi mrithi wake madaraka kwa njia ya amani.
Bw Joseph Kabila aliingia madarakani mwaka 2001 baada ya kuuawa kwa babake, Laurent Kabila
Mamia ya watu walishiriki maandamano hayo ya Jumatatu mjini Kinshasa
Post a Comment