Moja
ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya
ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation)
toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere saa sita na
robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
20
Septemba, 2016, Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa
ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere Jijini Dar es salaam
ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege
hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na
kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya
inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza
baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard
Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja
na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi
rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
Moja
ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya
ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius K. Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine
wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam
leo Septemba 20, 2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha
Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya
kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius K. Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba
20, 2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine
wakiwa kwenye Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa
ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam
leo Septemba 20, 2016.
Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakiwa kwenye Ndege hiyo.
Rubani wa Ndege hiyo akiweka mambo sawa baada ya kutua.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho, Mkurugenzi wa Kampuni ya
Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu pamoja na marubani
waliokuja na ndege hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya
kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo Septemba 20,
2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep
Sandhu mara baada ya Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam
leo Septemba 20, 2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akizungumza na vyombo vya habari
mara baada ya kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam
leo Septemba 20, 2016. PICHA NA IKULU.
Post a Comment