0



Hivi sasa watu wengi wakiwa mbali na simu ya mkononi kwa muda huhisi wamekosa kitu muhimu.

Simu ya mkononi hivi sasa ina nafasi muhimu na yenye faida kubwa katika maisha yetu ya kila siku.

Hapo zamani kidogo watu walikuwa wakiwasiliana kupitia simu ya mezani iliyokuwa katika sehemu moja maalum, leo simu ya mkononi daima iko pamoja nasi kila sehemu tulipo.


Mbali na kusahilisha mawasiliano baina ya wanadamu, simu ya mkononi inaendelea kutumika kufanya kazi mbali mbali kadiri teknolojia inavyozidi kustawi.

Kutuma au kupokea jumbe fupi sambamba na picha na taswira ni kati ya kazi za kimsingi za simu za mkononi. Mbali na hayo simu za mkononi pia zina programu kadhaa za michezo ambayo hutumiwa wakati mtumizi ana muda wa ziada kwa mfano akiwa ndani ya gari n.k.

Kwa ujumla ni kuwa urahisi wakupatikanakilamtu,mawasiliano mapana, kuongeza kasi ya kazi nyingi, kuondoa wasi wasi, kupunguza msongamano katika maeneo kama vile benki ni moja kati ya faida nyingi za simu za mkononi.

Jambo hili hasa linahisika zaidi katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania ikiwemo ambapo kumeenea mfumo wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi.

Mfumo huu ulioanza kutumiwa kwa mara ya kwanza nchini Kenya, duniani umepelekea huduma za benki kufika katika kila kona na kila kijiji katika nchi hizo za Afrika Mashariki.

Kizazi kipya cha simu za mkononi au smartphone yaani simu erevu zimepelekea mawasiliano ya intaneti kuingia katika duru mpya.

Watumiaji wengi wa simu erevu au smartphone katika maeneo mbali mbali duniani hutumia simu hizo kuingia katika intaneti na mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, viber, whatsapp, line, imo, telegram, instagram na mitandao mingine mingi ya kijamii ambayo inatumiwa kwa kiasi kikubwa na wanadamu wa karne ya 21.

Uwezo wa simu za mkononi hasa smartphone umeimarika kwa sababu mbali na kuwa na uwezo wa kutumia intaneti ya kasi, simu hizo zina kamera zenye uwezo mkubwa na mzuri wa kuchukua video na picha.

Simu za mkononi pamoja na kuwavutia watumiaji wengi duniani, lakini sawa na teknolojia zingine za kisasa za habari na mawasiliano, nazo pia ni upanga wenye ncha mbili kwani zina faida kubwa sana kwa mtumizi na pia zinaweza kuwa na madhara na athari hasi kiafya, kijamii na kimaadili na yote hayo yanategemea utumiaji wa chombo hicho muhimu.

Kuhusu madhara ya afya ya kimwili, simu za mkononi hasa zile aina ya smartphone au simu erevu, sawa na vifaa vingi vya kielektroniki huwa na miale au mawimbi ya kielektroniki ambayo yamkini yakahatarisha afya ya mwanadamu.

Wataalam waliofanya uchunguzi wamebaini kuwa miale na mawimbi ya simu za mkononi huwa na athari haribifu kwa afya ya mwanadamu.

Ingawa bado kuna haja ya kufanyika utafiti mpana na wa kina zaidi kuhusu madhara hayo, lakini matokeo ya awali ya uchunugiz ni sababu tosha ya kuwa na tahadhari kuhusu utumiaji kupita kiasi wa simu za mkononi.

Kwa msingi huo, katika dunia ya sasa ambapo tunatumia simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektronik tunapaswa kuzingatia na kutilia maanani madhara haribifu ya miale na mawimbi ya kielektroniki yenye madhara kwa afya.

Wataalam wamebaini kuwa, kuzungumza kwa muda mrefu kupitia simu za mkononi kunaweza kuwa na athari haribifu kwa uwezo wa ubongo kuhifadhi mambo.

Hivi sasa madaktari wanachunguza athari haribifu za mnunurisho wa simu za mkononi katika ubongo wa mwanadamu.

Utumiaji wa mara kwa mara wa simu ya mkononi na kuzungumza kwa muda wa zaidi ya dakika 20 ni jambo linaloweza kuongeza hatua kwa hatua joto katika ubongo na hilo husababisha muundo wa kibiolojia wa ubongo.

Kati ya madhara ya hali hiyo ni kupungua uwezo wa kusikia. Kiwango cha kuathiriwa sikio hutegemea pia umbali uliopo baina ya simu ya mkononi na sikio linalotumika kusikilza mazungumzo.

Kadiri simu inayokukaribia ndivyo miala na mawimbi ya chombo hicho huwa na athari mbaya zaidi.

Kwa ujumla ni kuwa zaidi ya asilimia 70 ya mawimbi ambayo huingia ubongoni kutoka katika simu ya mkononi huwa na athari mbaya katika utenda kazi wa ubongo wa mwanadamu.

Hata baadhi ya wataalam wanaamini kuwa, utumiaji wa mara kwa mara na wa muda mrefu wa simu ya mkononi huongeza kwa kiasi uwezekano kuibuka uvimbe wa ubongo (brain tumor).

Kwa msingi huo uwezekano wa kuibuka uvimbe wa ubongo huwa juu zaidi kwa wanaotumia simu za mkononi.

Kwa hivyo, kama walivyosema wataalam utumiaji wa muda mrefu wa simu za mkononi na hivyo kulengwa kwa muda mrefu na mawimbi pamoja na miale ya kielektroniki ni jambo lenye madhara makubwa kwa afya ya mwandamu.

Kati ya madhara tunayoweza kuashiriki hapa ni kama vile kpungua uwezo wa ubongo kuhifadhi mambo, kuhisi uchovu, kukosa usingizi, saratani, uvimbe wa ubongo, utasa na ugumba.

Athari hizi mbaya za simu za mkononi hasa huwaathiri zaidi wagonjwa, watoto na wazee.

Majaribio yaliyofanyika katika maabara yameebaini kuwa utumiaji kupita kiasi simu za mkononi hupelekea pia kuongezeka shinikizo la damu, na maumivu ya kichwa.

Wataalam wanashauri kuwa usiweke simu karibu na moyo au eneo la kiuno.

 Inashauriwa pia kuwa simu ibebwe kwenye mfuko ambao hauko katika nguo ili athari zake mbaya zipungue.
Swali la kujiuliza: Je, wewe hutumia dakika ngapi kuzungumza na simu?, Simu yako huwa unaiweka wapi? Wakati wa kulala Je?

Post a Comment

 
Top