Mchezaji wa timu ya Sido fc akikokota mpira
Mchezaji wa timu ya Kipule fc akiweka mpira sawa kwa kupiga faulo lakini mchezaji huu hakuvaa viatu katika mchezo huu ni moja ya changamoto za timu za wilayani Liwale mkoani Lindi.
Leo ikiwa julai 7 mashabiki wa soka wilayani Liwale walishudia mchezo wa mpira katika ligi ya Liwale super Cup ambapo kulikuwa na mchezo uwanja wa wilaya kati ya timu ya Sido fc dhidi ya Kipule fc.
Mchezo huu ulikuwa na watazaji wengi katika kipinda cha kwanza timu ya Kipule fc iliweza kuongoza goli mmoja lililofungwa na Haji Mtutuma namo dakika ya 44 na goli lililodumu mpaka dakika 45 ya kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili mchezo ulikuwa wa kasi huku kila timu ikitafuta nafasi ya kupachika goli lakini katika dakika ya 73 Hamisi Mrope aliweza kuisawazishi goli timu yake ya sido fc na dakika ya 89 Hamza Lipupu aliweza kupachika goli la pili la ushindi kwa timu ya Sido fc,dakika 90 zinapuliza kipenga cha kumaliza mchezo matokeo yalikuwa Sido fc 2-1 Kipule fc.
Kocha wa Sido fc Mohamedi Hema aliweza kuzungumzia mchezo kwa kusema mchezo ulikuwa mgumu richa ya kushinda nae kocha wa Kipule fc Sudi Masudi alisema mchezo ulikumbwa na kasoro kwa waamuzi wa mchezo huku akiwalalamikia waamuzi kwa kuchezesha mpira kwa kuangalia timu inatokea wapi ameomba waamuzi wachezeshe mpira kwa kufuata sheria za soka bila kujali timu inatokea sehemu fulani.
Post a Comment