0

Sheria za madereva wa magari Kabla ya kuendesha

  1. LAZIMA uwe na leseni halali ya udereva kwa daraja la gari unaloendesha (unaweza kuendesha kwa kutumia leseni halali ya kimataifa au leseni ya kigeni kwa miezi sita baada ya kufika Tanzania kwa mara ya kwanza).
  2. LAZIMA uwe unajisikia vizuri - usiwe mgonjwa au umechoka.
  3. LAZIMA uweze kuona vizuri (uweze kusoma kibao cha namba za gar kutoka umbali wa mita 20) - iwapo unahitaji kuvaa miwani au lenzi ili kuona
  4.  LAZIMA uvae wakati wa kuendesha - usitumie miwani ya jua usiku au kukiwa na mwanga mdogo.
  5. USISHINDWE kuliongoza gari kwa sababu ya kunywa pombe au kutumia dawa za kulevya njia pekee ya kuwa na uhakika na jambo hili ni kutokunywa pombe au kutumia dawa yoyote ya kulevya.
  6. LAZIMA uhakikishe kuwa, wakati watoto wadogo wamo kwenye gari, wawe viti vya nyuma ya gari, wako chini ya usimamizi wa watu wazima, na milango imefungwa (tumia vidhibiti mtoto) – inashauriwa kuwa uweke na kutumia vizuizi vya mtoto vinavyofaa (kibebea mtoto, kiti cha mtoto, au kiti cha busta kwa watoto wakubwa).
  7. LAZIMA ujifunge mkanda – hili lifanywe na abiria wa kiti cha mbele pia – inashauriwa sana kuwa abiria wa viti vya nyuma pia wajifunge mikanda.
  8. LAZIMA urekebishe kiti chako na vioo ili uweze kuendesha vizuri, na uweze kuona sehemu zote za gari.
  9. LAZIMA uchukue:
  10. leseni yako ya udereva
  11. cheti halisi cha usajili wa gari au nakala halisi
  12. LAZIMA ubandike kwenye gari:
  13. kibandiko/stika ya leseni halali ya gari
  14. kibandiko/stika ya bima (isipokuwa kwa magari yanayomilikiwa na Serikali)
  15. Gari lako LAZIMA:
  16. liwe katika hali nzuri ya kiufundi
  17. iwe ndani ya eneo linaloruhusiwa
  18. liendane na viwango vyote, vya utengenezaji (Shirika la Viwango Tanzania)
  19. liendane na kikomo cha idadi ya abiria ambao wanaweza kubebwa 17
  20. ipakie mizigo kiusalama, kulingana na kanuni – hakikisha kuwa mizigo yoyote iliyobebwa iko salama na isining’inie nje na isisababishe hatari weka alama ya tahadhari mwishoni mwa mzigo uliozidi sehemu ya nyuma ya gari.
  21. Lilingane na kanuni za kiwango cha juu cha uzito. Ukaguaji wa kila siku (magari)
  22. Kagua magurudumu kama yako kwenye hali nzuri na nati ziko salama
  23. Kagua kuona kuna mafuta ya kutosha, mafuta ya breki, maji, na kiosha kioo cha mbele
  24. Kagua kuwa waipa za kioo cha mbele zinafanya kazi
  25. Kagua matairi, ikiwa ni pamoja na tairi la akiba, kwa uharibifu, kina cha tredi (kima cha chini kilichopendekezwa ni: mm3) na upepo
  26. Kagua kuwa taa na indiketa zinafanya kazi vizuri
  27. Kagua kuwa honi inafanya kazi vizuri
  28. Kagua kuwa vioo vyote ni safi ndani na nje, na kuwa vioo na viashiria ni safi
  29. Kagua nje ya gari kwa ubovu au uharibifu
  30. Kagua kuwa vifaa na jeki vipo na vinafanyakazi vizuri
  31. Kagua kama kuna mngurumo usio wa kawaida wakati injini inafanya kazi.
  32. Usiendeshe wakati umechoka au unaumwa. Kuendesha kunaweza kukufanya ujisikie usingizi.


Hili linaweza kuepukwa kwa kuhakikisha kuwa kuna hewa ya kutosha kwenye gari lako. Iwapo unajisikia kuchoka wakati wa kuendesha tafuta sehemu salama ya kusimama na pumzika.

 Kunywa vikombe viwili vya kahawa kunaweza kukusaidia. Inashauriwa kuwa upumzike kwa dakika 30 kila baada ya kuendesha kwa saa 3.

Usiendeshe kwa zaidi ya saa 9 kwa siku. Epuka kuanza safari ndefu usiku sana.

Madereva wa magari ya biashara lazima wafuate kanuni za saa za madereva.

Usiendeshe wakati unaumwa. Iwapo unameza dawa muulize daktari wako au mfamasia kama ni salama kuendesha.

Iwapo utakuwa mgonjwa kwa muda mrefu au hujiwezi na daktari wako akisema si salama tena kwako kuendesha ipeleke leseni yako Polisi.

Usinywe pombe na kuendesha.

Pombe hupunguza mpangilio wako, kupunguza utendaji wako, kuathiri uamuzi wako wa mwendo, umbali na hatari, na kukupa hisia zisizo sahihi za kujiamini.

Hairuhusiwi kuendesha  18 ukiwa na kiasi cha pombe kwenye damu cha juu zaidi ya mg80/ml100 lakini uendeshaji wako unaweza kuathiriwa kabla hata ya kufikia kikomo hiki.

Kwa hiyo, ni vizuri kutokunywa kileo chochote kabla ya kuendesha.

Kumbuka kuwa inachukua muda kwa kileo kuondoka mwilini mwako, hivyo unaweza kutokuwa katika hali nzuri ya kuendesha jioni baada ya kunywa pombe wakati wa chakula cha mchana.

Madereva wa mabasi, daladala, na magari ya mizigo yanayotoa huduma za usafiri WASINYWE kileo chochote kabla ya kuendesha. Iwapo unajifunza udereva.

LAZIMA uwe na leseni halali ya dereva mwanafunzi, na wakati unaendesha LAZIMA uwe unaongozwa na mwalimu wa udereva aliyesajiliwa anayefanya kazi kwenye shule ya udereva iliyothibitishwa.

Iwapo unajifunza kuendesha pikipiki, skuta au baiskeli mota lazima uchukue mafunzo ya msingi kwenye shule ya udereva iliyothibitishwa kabla ya kuendesha barabarani - usibebe abiria nyuma.

Magari yote (pamoja na pikipiki na baiskeli mota) yanayoendeshwa na mwanafunzi LAZIMA yawe na kibao cha Mwanafunzi (L) kilichothibitishwa.

Post a Comment

 
Top