TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa
Selestine leo amemtambuisha kocha
mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa
mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea na waandishi wa habari,
Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira
wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha
hao wazawa wanaoanza kazi kesho
kujiandaa na mchezo wa marudiano
dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini
Kampala.
Mara baada ya kutambulishwa kwa
waandishi wa habari, Mkwasa amesema
anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi
hiyo ya kuingoza Taifa Stars na
msaidizi wake Hemed Morocco, na
kuomba watanzania kuwapa sapoti.
Mkwasa amesema cha kwanza
atakachokifanya na msaidizi wake
Morocco ni kurudisha imani ya
watanzania juu ya timu yao ya Taifa,
kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao
kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri
katika michezo inayowakabili.
Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha
wachezaji 26 watakaoingia kambini
kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma
tayari kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Wachezaji walioitwa ni makipa:
Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally
(Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam),
Michael Aidan (Ruvu Shooting),
Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba),
Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub
“Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani
(Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey
Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi
Banda (Simba), Salum Telela (Yanga),
Frank Domayo (Azam).
Viungo wa pembeni: Saimon Msuva
(Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus
Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano
“Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam),
Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid
Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally
(Mtibwa Sugar).
Wachezaji Juma Abdul (Yanga),
Mudathir Yahya (Azam) na Samwel
Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama
wachezaji wa akiba katika kikosi cha
timu ya Taifa kinachoingia kambini
kesho.
Katika hatua nyingine Mkwasa
ametangaza benchi la ufundi la Taifa
Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco,
kocha wa magolikipa Peter Manyika,
Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni,
mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku
mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd
Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza
majina ya daktari wa timu na mchua
misuli watakaoungana na kambi ya
Taifa Stars.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA
WA MIGUU TANZANIA (TFF)
miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa
Selestine leo amemtambuisha kocha
mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa
mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea na waandishi wa habari,
Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira
wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha
hao wazawa wanaoanza kazi kesho
kujiandaa na mchezo wa marudiano
dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini
Kampala.
Mara baada ya kutambulishwa kwa
waandishi wa habari, Mkwasa amesema
anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi
hiyo ya kuingoza Taifa Stars na
msaidizi wake Hemed Morocco, na
kuomba watanzania kuwapa sapoti.
Mkwasa amesema cha kwanza
atakachokifanya na msaidizi wake
Morocco ni kurudisha imani ya
watanzania juu ya timu yao ya Taifa,
kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao
kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri
katika michezo inayowakabili.
Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha
wachezaji 26 watakaoingia kambini
kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma
tayari kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Wachezaji walioitwa ni makipa:
Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally
(Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam),
Michael Aidan (Ruvu Shooting),
Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba),
Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub
“Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani
(Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey
Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi
Banda (Simba), Salum Telela (Yanga),
Frank Domayo (Azam).
Viungo wa pembeni: Saimon Msuva
(Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus
Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano
“Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam),
Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid
Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally
(Mtibwa Sugar).
Wachezaji Juma Abdul (Yanga),
Mudathir Yahya (Azam) na Samwel
Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama
wachezaji wa akiba katika kikosi cha
timu ya Taifa kinachoingia kambini
kesho.
Katika hatua nyingine Mkwasa
ametangaza benchi la ufundi la Taifa
Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco,
kocha wa magolikipa Peter Manyika,
Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni,
mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku
mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd
Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza
majina ya daktari wa timu na mchua
misuli watakaoungana na kambi ya
Taifa Stars.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA
WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Kocha Mkwasa (kushoto) na msaidizi
wake Hemed Morocco wakiongea na
waandishi wa habari.
wake Hemed Morocco wakiongea na
waandishi wa habari.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.