0
Na Mary Gwera
KATIKA mwendelezo wa maboresho ya
utoaji wa huduma ya haki nchini,
Mahakama ya Tanzania inaendelea
kufanya jitihada mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kukutana na wadau pamoja
na Washirika mbalimbali wa maendeleo
ili kupata maoni yao juu ya uboreshaji
wa huduma zake.
Akiongea na Waandishi wa Habari
mapema jana, katika Warsha
iliyoandaliwa na  Mahakama
ikishirikisha Ugeni kutoka Benki ya
Dunia na Wawakilishi kutoka Jumuiya ya
Wafanyabiashara kutoka, TRA, Umoja
wa Taasisi za Kifedha,MOAT, TIRA,
TCRA n.k iliyofanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam, Bw.
Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania alisema
Mahakama imekuwa katika mchakato wa
maboresho na washirika mbalimbali wa
Maendeleo na wadau wa utoaji haki ili
kuboresha huduma zake.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu,
Mahakama ya Tanzania (wa kwanza
kushoto), Bw. Waleed Malik, Mwakilishi
kutoka Benki ya Dunia (wa pili kushoto),
Bi. Neema Ndunguru, Mkurugenzi wa
Mazingira ya Biashara (PDB) pamoja na
wawakilishi kutoka Benki ya Dunia
wakiwa meza kuu wakati wa Kikao cha
majadiliano katika ya Mahakama na
Wadau wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
kupata maoni juu ya maboresho ya
huduma za Mahakama. (IMG. 7436)

Post a Comment

 
Top