0

Mwalimu mmoja mkuu amekiri kufanya ngono
na wavulana wawili wenye umri mdogo.
Anne Lakey, mwenye umri wa miaka 55,
kutoka eneo la Stanley, katika kaunti ya
Durham, amekanusha makosa 13 dhidi yake
ya kufanya matendo ya aibu kwa kushikashika
sehemu za siri wavulana wawili miaka ya
themanini.
Lakini jaji katika mahakama ya Teesside
Crown, alimpata na hatia ya makosa hayo
yote baada ya kesi iliyochukua majuma
mawili.
Mahakama ilisikiza ushahidi wa namna
alivyokuwa akitenda matendo hayo ya kuudhi
na aibu katika kipindi cha miaka mitatu
mfululizo.
Atahukumiwa jela Jumatano wiki hii.
Mahakama iliambiwa kuwa baadhi ya makosa
yalifanyika pale Lakey alipokuwa mwalimu wa
kufundisha somo la historia akiwa na umri wa
miaka 20.
Lakey, ametajwa na waendesha mashtaka
kama "mnyama wa ngono", alimlenga
mvulana wa miaka 15 na waathiriwa wengine
wawili wenye umri wa kati ya miaka 13 au 14.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo, mmoja wa
waathiriwa aliwaambia majaji kuwa mama
huyo wa mtoto mmoja alimuondolea ubikra
pale alipomtaka amtizame alipokuwa akioga.
Lakey alifanya kazi yake ya ualimu kwa
ushindi mkubwa kwani alisifiwa mno kwa
kufaulisha Shule hiyo iliyokuwa imedorora
kielimu na kuifanya mojawepo ya shule
iliyopata mafanikio makubwa.
Lakini mnamo mwaka 2012, mojawepo wa
waathiriwa alituma ujumbe kwa njia ya barua
pepe hadi shuleni humo, iliyosababishwa
afutwe kazi na kisha polisi wakafahamishwa.BBC
Headteacher

Post a Comment

 
Top