0


Mawaziri wa Mambo
ya nje wataka vita
iishe Ukrain
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Ukraine
wameelezea wasiwasi kuhusu hali ya
usalama Mashariki mwa Ukraine na kutoa
wito wa kusitishwa mapigano kuruhusu
mchakato wa kisiasa kusonga mbele.
Mawaziri wakizungumzia mzozo wa
Ukraine mjini Paris
Mawaziri hao wamekutana katika juhudi za
kujaribu kuyaokoa makubaliano ya
kusitisha mapigano nchini Ukraine, ambayo
yalitiwa saini mjini Minsk-Belarus mwezi
Februari. Akizungumza kwa niaba ya
wenzake, waziri wa mambo ya nchi za nje
wa Ufaransa Laurent Fabius amesema
wametaka mapigano yasitishwe mara moja
katika eneo la Donbas, akimaanisha ukanda
wa mashariki mwa Ukraine unaokabiliwa
na vita.
Mwenzake wa Ujerumani, Frank-Walter
Steinmeier amesema anayo matumaini
kwamba mapigano yatasitishwa katika mji
wa Shyrokyne ulio umbali wa kilomita 23
mashariki mwa mji muhimu wa Mariupol
katika jimbo la Donetsk.
Steimeier amesema, ''Ninayo matumaini
kwamba usiku wa leo tumepiga hatua
mbele, lakini tutategemea utashi wa
Ukraine na Urusi kuweza kushirikiana. Si
Ufaransa wala Ujerumani zenye uwezo wa
kuutanzua mzozo huo, bali pande
zinazohusika zinatakiwa kuheshimu
makubaliano ya mjini Minsk.''
Suluhisho mikononi mwa Urusi na Ukraine
Waziri Steinmeier ameendelea kusema
kuwa suluhisho haliwezi kutokana na
juhudi za kisiasa pekee, na kuongeza kuwa
wanahitaji utaalamu wa kijeshi wa Shirika
la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya,
OSCE, kuweza kupata mpango mzima wa
namna mkataba wa Minsk ulivyokiukwa na
vikosi vya serikali ya Ukraine pamoja na
waasi wa mashariki wanaoegemea upande
wa Urusi.
Mawaziri hao wamekutana mara kadhaa
mnamo miezi michache iliyopita, kukiwa
na shutuma za kukiukwa ma makubaliano
ya kusitisha vita yaliyotiwa saini mjini
Minsk. Mazungumzo yao bado hayajaweza
kuleta tija, katika kushinikiza makubaliano
hayo yatekelezwe kikamilifu.
Marekani kupeleka silaha nzito Ulaya
Mashariki
Kuhusiana na mvutano kati ya Urusi na
nchi za Magharibi uliosababishwa na
mzozo huo wa Ukraine, Marekani imesema
itaanza kupeleka silaha nzito nzito katika
mataifa matatu ya Ulaya Mashariki,
ambazo ni wanachama wapya wa Umoja
wa Kujihami wa NATO.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashton
Carter ameyatangaza hayo jana katika
mkutano na waandishi wa habari pamoja
na mawaziri wenzake wa ulinzi wa nchi
hizo za eneo la Baltic. Carter amesema
silaha hizo zitajumuisha vifaru, magari ya
kivita pamoja na mizinga, na kuthibitisha
kuwa Estonia, Lithuania, Latvia, Bulgaria,
Romania na Poland zimekubali kuvipokea
vikosi vitakavyozisindikiza silaha hizo.
''Ingawa hatutaki vita baridi vipya na
Urusi, sembuse vile vya moto na nchi hiyo,
tutasimama kidete kuwalinda washirika
wetu'' amesema waziri wa ulinzi wa
Marekani Ashton Carter.
Mkutano huo kati ya Carter na wenzake wa
nchi za Baltic, umefanyika kwenye
mkutano wa NATO wa ngazi ya mawaziri,
ambao unafanyika leo katika mji mkuu wa
Estonia, Tallinn.
Wachambuzi wanasema hatua hiyo ya
Marekani, inatuma ujumbe kwa washirika
wake pamoja na Urusi, kwamba bado nchi
hiyo ni taifa kubwa, ambalo linao uwezo
kijeshi kukabiliana na kitisho cha Urusi
Mashariki mwa Ulaya.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top