
Ni vita kwa Simba iliyo katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa
ligi ikiwa na pointi 16 inaposaka ushindi na pointi tatu leo dhidi ya
Coastal Union ya Tanga ili ipande kwa mara ya kwanza na kuingia tatu
bora.
Simba haijagusa tano bora kwenye msimamo, ila kama
itashinda leo itavunja mwiko kama ilivyotokea kwa Yanga ilipoifunga
Coastal Union 1-0 Jumatano na kukaa kileleni kwa mara ya kwanza.
Timu hiyo inaikabili Coastal Union ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakani, ikiwa na lengo la kushinda na kupanda juu.
Mechi nyingine za leo zitakuwa ni; JKT Ruvu na
Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Ruvu Shooting, ugenini
kuikabili Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, Ndanda wataikaribisha
Stand United, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na Kagera Sugar wakiwa
uwanja wao mpya, Kambarage Shinyanga kuikabili Mgambo JKT.
Hata hivyo, haitakuwa kazi rahisi kwa Simba
kushinda leo dhidi ya Wagosi wa Kaya, ambao wanaugulia maumivu ya
kufungwa 1-0 na Yanga na hawako tayari kupoteza mchezo mwingine
kirahisi, wakiwa nyumbani.
Kocha Goran Kopunovic alisema mechi hiyo itakuwa
ngumu kwani wapinzani wao wanatumia mabavu uwanjani, lakini watapambana
ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Kopunovic aliisoma Coastal Union wakati ikicheza
na Yanga, ambako aligundua mambo kadhaa, likiwamo la jinsi timu hiyo
inavyocheza soka la nguvu na ubabe.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.