0

Na.Ahmad Mmow, Kilwa.
Mgogoro wa ardhi umeibuka wilayani Kilwa mkoani Lindi, Wananchi na Serikali ya kijiji cha Makangaga ,kukosoa na kulalamikia amri ya serikali iliyotolewa na mkuu wa wilaya hiyo, Juma Njwayo inayowataka wananchi 149 wasiendelee kufanya shughuli za kilimo kwenye eneo linalodaiwa kuwa ni la hifadhi. 

Nangurukuru
Wakizungumza mwanzoni mwa wiki hii kwa nyakati na maeneo tofauti, kijijini hapo, mbele ya mbunge wa jimbo la Kilwa kusini, Seleman Bungara. Wajumbe wa serikali ya kijiji kupitia kikao cha ndani, na wananchi kwenye mkutano wa hadhara waliita amri hiyo niyauonevu, kwa madai kuwa haikuzingatia ukweli wa historia na mipaka ya kijiji hicho.

Walisema eneo walilozuiwa wasilime, sio la hifadhi kama inavyodaiwa na mkuu huyo wa wilaya.

Mzee Ali Mnyimage aliyedai alizaliwa, kukulia na kuishi kijijini hapo, alisema anaifahamu mipaka na hata eneo ambalo linadaiwa nilahifadhi analijua kutokana na wataalamu wa halmashauri ya wilaya hiyo kwenda kupima mipaka ya kijiji hicho kabla ya kuingia kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Mzee Muhibu Kibwanga, alisema wanashangazwa na amri hiyo na kuiita ya uonevu. Kwa madai kuwa eneo ambalo wametakiwa waliache ndilo ambalo alipewa mwekezaji ili alime shamba la miwa. Nakuongeza kuwa upimaji wa wamipaka ya kijiji hicho ulisababishwa na kijiji kuingia kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi baada ya mwekezaji huyo kuomba kuwekeza.
"Mwekezaji huyo alitokea wilayani hukohuko,na halmashauri inamjua alitokea wapi,napale palisemwa kwa ajili ya uwekezaji "tulikutana hapahapa kwenye mkutano wa kijiji akaruhusiwa alime shamba la miwa, sasa hiyo hifadhi imeanza lini na kwanini kwetu sisi tu nasiyo yule mwekezaji," alihoji mzee huyo.

Bwana Athumani Said, alisema sababu zilizotolewa na serikali kuhusiana na eneo hilo hazina ukweli wowote. Kwamadai kwamba anaifahamu mipaka kutokana maofisa wa mawakala wa misitu waliokwenda mwaka 2014 na 2015 kujiridhisha kuwa eneo hilo siyo la hifadhi na kijiji hicho kimepimwa.

Nakwamba eneo wanalolima ni tofauti na mto Nyange ambao unatajwa kuvamiwa na wananchi hao kwa shughuli za kilimo. 
Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina Mohamed Abdallah alisema amri hiyo inapingana na maelezo ya wataalamu wa serikali waliokwenda kupima na kuweka mipaka. Kwamadai yeye ni miongoni mwa wananchi walioshuhudia upimaji uliofanywa na watalaamu waliotoka wilayani.
"Hawakusema kama eneo lile nihifadhi ya serikali, hawawezi kuonesha kwenye ramani jambo linalosemwa na mkuu wa wilaya,"alisema Mohamedi. 

Awali wajumbe wa serikali ya kijiji hicho wakiwa na mbunge huyo kwenye kikao chandani, walisema eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 29500, ambazo kati ya hizo ekari 779
zimeshalimwa na wananchi hao, sio hifadhi. Bali lilitengwa kwa ajili ya uwekezaji. Ambao pia wasema kijiji hicho kimepimwa na wataalamu kutoka kwenye halmashauri ya wilaya ya Kilwa, wakati kilipoingia kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi.


Walisema kwa kuzingatia ukweli huo ndio sababu sehemu ya eneo linalotajwa na mkuu wa wilaya kama hifadhi waliridhia kumpa mwekezaji. Wajumbe hao walisisitiza na kushauri mgogoro huo utakwisha iwapo halmashauri ya wilaya hiyo itaonesha na kukabidhi ramani ya kijiji hicho ambayo mpaka sasa hawajapewa. 

Alipoombwa na Mtandao huu wa Lindiyetu.com ili aeleze analolifahamu kuhusu kuhusu maelezo hayo. Menyekiti wa halmashauri hiyo, Abou Mjaka alikiri kuwa wananchi hao wamekatazwa na mkuu wa wilaya, wasilime kwenye eneo hilo kwa madai kuwa ni hifadhi.

Alisema yeye ni miongoni mwaviongozi walikwenda katika kijiji hicho nakupata maelezo ya wananchi na viongozi wa kijiji hicho. Hata hivyo mwenyekiti huyo alisema hawezi kusema ni nani kati ya mkuu wa wilaya na wananchi hao yupo sahihi. Bali amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo ampelekee ramani ya kijiji hicho kwani kilishapimwa na kuingia kwenye mpango bora wa matumizi ya ardhi.
"Ukweli wa nani yupo sahihi utajulikana baada ya kupata ramani hiyo ambayo imeainisha na kuonesha kila kitu,"kama nikweli itaonekana kuwa eneo hilo siyo la hifadhi hatutakubali wananchi hao waondoke hasa kwa kuzingatia wamepoteza nguvu na muda, hawawezi kuwa na njia mbadala ya kuwahi msimu huu wa kilimo,"alisema Mjaka.

Akizungumzia mgogoro huo kwaniaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Erenest Mwakang'ata alisema nivigumu ofisi yake kuutolea majibu mgogoro huo. Ingawa alikiri kuwa kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vilivyopo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi. Ambapo pia alikiri kuwa ufumbuzi mgogoro huo unaweza kupatikana baada ya kupata kitabu cha matumizi bora ya ardhi ambacho kinaramani yakijiji hicho.
"Hicho kitabu kimeshafuatwa ofisi ya tume ya matumizi bora ya ardhi, kwa sasa kunakila sababu ya kutii na kuheshimu amri ya serikali kuhusu eneo hilo, iwapo ufumbuzi ni ramani basi itakuja,"alisisitiza Kaunda.

Hata hivyo mmoja wa watumishi ndani ya halmashauri hiyo ambae hakutaka jina lake liandikwe kwamadai kuwa siyo msemaji wa halmashauri hiyo, alisema wananchi hao huenda wapo sahihi kusema eneo walilolima sio la hifadhi. Kwa madai kuwa wajumbe wa serikali ya kijiji hicho wanaujua ukweli kutokana na kushuhudia hatua zote za upimaji.

Hatahivyo hawanabudi kutii amri hiyo. Taarifa kutoka wilayani humo zimeeleza kuwa mkuu huyo wa wilaya alikwenda katika kijiji hicho mwaka jana, tarehe 14 disemba na kuwapa amri wananchi waliolima kwenye eneo hilo waondoke kabla ya tarehe 24 ya mwezi huo. Ambapo hadi sasa ekari hizo 779 hazijapandwa mbegu.

Post a Comment

 
Top