0


RAIS-wa-Rwanda-Paul-Kagame


Na.Raidhani Mohamedi, Liwale - Lindi TZ 
         Nianze kutumia fursa hii kwa kumshukuru sana Mwenyezimungu na Viumbe wengine ambao tunawamini kwa mujibu wa imani zetu kwa kutuwezesha kuona na hatimaye kuuishi Mwezi March, Mwezi ambao umekuwa na mitazamo miwili tofauti inayotogemeana na mazingira ya eneo husika,
Mtazamo wa kwanza ni kwamba wapo baadhi ya Watu wanaoamini kuwa Mwezi huu ni wa majanga na madhara zaidi hasa kutokana na uwepo wa mvua nyingi ambazo mara kadhaa zimekuwa zikiambatana na radi pamoja na upepe mkali, wakati dhana nyingine ni wale waodhani kuwa mwezi huu ni wa mafanikio zaidi kutokana na uwepo wa Mvua hizohizo ambapo wanaamini kuwa zitawasaidia kwenye shughuri mbalimbali hasa Wakulima, na Wafugaji. Lakini pamoja na yote ni ukweli usiopingika kuwa tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa wakati huu
RAIS KAGAME ANAPOCHEZA 'SINEMA' RWANDA
Sasa naomba nielekee moja kwamoja kwenye agender yangu kubwa niliyoamua kuiwasilisha kwenye ukurasa huu, Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza maswali yafuatayo kuhusu Rwandwa, Hivi Kwanini Rwanda inaongozwa na Rais Paul Kagame hadi sasa?, Je, ni kweli kwamba Wanyarwanda wanamhitaji sana Kagame au Kagame anawahitaji sana Wanyarwanda?, Hivi Rwanda kabla ya Kagame ilikuwaje na Je, Siku moja Kagame akiamua kuondoka madarakani Taifa hilo lililo jirani na Tanzania litakuwaje?
Haya ni baadhi tu ya maswali mengi mbayo nimekuwa nikijiuliza lakini kwa muda wote huo nimekosa majawabu thabiti yatakayoniwezesha kuitazama Rwanda kwa Jicho la tatu.
Nafika wakati najiuliza kuhusu Jamii ya Wahutu iliyopo pale Rwanda na ile iliyokuwepo miaka ile ambayo ilionekana si chochote si lolote, inawezekana hadi kufikia sasa usinielewe sana lakini ngoja nikurudishe miaka kadhaa huko nyuma
Miongoni mwa Jamii iliyokuwa ikidharauliwa enzi hizo pale Rwanda ni Wahutu, Wahutu hawa licha ya kuwa na idadi kubwa sana ya Wanyarwanda ambapo kati ya Wanachi wa Rwanda Million 11, basi kati yao asilimia 80 ni Wahutu, lakini licha ya uwingi wao Wahutu walikuwa kwenye wakati mgumu sana ukiitaja miaka 23 huko nyuma, Nakumbuka wakati ule Jamii ya Wahutuw alilazimika kukaa juani kwa masaa mengi zaidi wakisubiri hotuba ya Dakika 20 ya Rais Paul Kagame
Wahutu walikuwa wanauwawa, Vita, Mapigano yakawaida vilikuwa vikirepotiwa kila uchwao kwenye Jamii hiyo hasa pale walipokuwa wanapogusa au kuingia kwenye himaya za askari wa Iwawa, ama kwahakika Wahutu walikuwa hawatendewi hutu pale Rwanda
Lakini si hayo tu Rais Paul Kagame wasasa ananitofautisha sana na wa wakati ule, Katika Kipindi cha majuzi tu Taifa hilo lilikuwa kwenye uchaguzi mkuu waliouita wa kidemokrasia zaidi ambapo matokeo ya mwisho Kagame alitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo kuwa ni mshindi, Licha ya ushindi huo bado Vyama vya Upinzani vimekuwa vikilalamikia kuminywa kwa Demokrasia, Tume ya taifa kutokuwa huru kwenye maamuzi, kutopazwa ipasavyo kwa sauti za Wanasiasa na wanaharakati wengine wa maendeleo hali iliyopelekea hata Mwanadada shupavu Dianne Rwigara ambaye alitia nia ya kuwania Urais wa nchi hiyo licha ya kutopitishwa na tume ya taifa ya Uchaguzi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutpkidhi vigezo vilivyowekwa lakini hata hivyo yeye na familia yake akiwemo Mama yake Mzazi Dianne Rwigara waliishia kwenye mikono ya vyombo vya dola, hiyo ndiyo siasa na Demokrasia ya Rwanda ya Paul Kagame
Nina mengi ya kuzungumza kupitia ukurasa huu lakini bado natengeneza maswali hivi ni kwanini Shule, maduka, masoko, makanisa, Ofisi za baadhi ya taasisi za kiserikali na zile zisizokuwa na kiserikali zote wakati mwingine zinalazimika kufungwa?, Je ni kwamba wakati huo hazina watumiaji au?, na kama wapo wamekwenda wapi?, na kwanini watoke wote?, maswali haya yote hayana majawabu kwakuwa wahusika pia hawajuwi kinachoendelea kuhusu hilo ingawa dhana ya walio wengi ni muendelezo wa kuminywa na kufungwa midomo kwa wasio na sauti
Vyombo vya habari pale Rwanda navyo najuwa vinapambana sana na shubiri ya Kagame hasa panapokuja hoja za kutaka kumkosoa yeye binafsi na hata serikali anayoiongoza, Rwanda sasa inatazamwa tofauti kabisa na asasi za kimataifa
Binafsi maswali yangu pia yanatua kwenye taswira za muonekano wa stayle ya Vazi la Korea Kusini, Hivi kinaendelea nini kati ya Rwanda ya Paul Kagame na Korea Kusini?, Maana haiwezekani kwenye mazingira ya kawaida tu Wanyarwanda walio wengi weweze kupendekeza kutumia style ya Korea Kusini, Kwanini wasibuni la kwao, nani aliwapa wazo hilo na kwanini?
Wakati nikijiuliza maswali haya yote, kuna rafiki yangu mmoja ananisogelea na kuniambia kuwa 'nyuma ya pazia' kuna kitu kinnaendelea na ni vigumu kukifahamu kwa haraka.
Hali hii ya 'ufinyu' wa Demokrasia na Siasa imekuwa ikitajwa sana hasa kwa Watawala wengi wanaobahatika kuongoza mataifa mengi Duniani lakini Afrika imekuwa kinara wa hili. Leo hii jina la mtu kama Idd Amin Dada hakuna asiyelijuwa kwenye historia ya pale Uganda na hata nje ya mipaka, huyu mtu alikuwa Dikteta wa moja kwa moja na amepoteza maisha ya wengi zaidi kwa wakati ule.
Na ukitaja Taifa la Uganda ambalo kwasasa linaongozwa na Rais Yoweri Kaguta Muiseven ambaye naye analalamikiwa kutawala kimabavu nchi hiyo, halijawahi kupata Rais wa kung'atuka madarakani kwa hiari badala yake wenyewe wamekuwa na Desturi ya 'kunyang'anyana' madaraka kutoka utawala wa mmoja hadi mingine, ni majuma kadhaa yaliyopita Bunge la nchi hiyo limeondoa ukomo wa Rais, hii yote imetokea kwakuwa Kipindi cha utawala kwa Rais Museven kinaelekea ukingoni hivyo kwasasa kuondoa huko ndio kusema kwamba sasa ana nafasi zaidi ya kuwatumikia Waganda, suala ambalo lilipingwa sana na Wafuasi wa Vyama vya upinza hali iliyopelekea kususia Bunge wakati mjadala huo ukiendelea lakini kama ule usemi usemavyo 'Papa ni papa, hawezi badilika mbele ya kambare au sato' mwisho wa Siku Sheria ikapita nasasa iko tayari kufanya kazi,
Je, nikikukumbusha ya hapa Majuzi tu kule Afrika Kusini ambako Jacob Zuma ameitwa mstahafu bila ya kutarajia, Vipi kuhusu Zimbabwe kwa Babu Robert Gabriel Mugabe nayeebila matakwa yake sasa anaitwa mstahafu, nina mifano mingi sana lakini itoshe kusema kuwa hii ndio Afrika
Nirejee tena kule Rwanda kwa Rafiki yangu kipenzi Rais Paul Kagame, kwasasa nimpongeze sana Kagame kwa kunitengenezea maswali na majibu, Kagame wa miaka 23 iliyopita sio huyu wa sasa. Kagame sasa anawathamini sana Wahutu, Kagame anawahitaji sana Wahutu hadi kufikia hatua ya kutumia Picha zao kwenye muonekano wa shughuri zake
Wahutu wenyewe wanajuwa kinachoendelea hasa wale waliokuwepo miaka 23 nyuma, Wanyarwanda nao wanajuwa na Kagame mwenyewe na Serikali yake pia anajwa.
Ndio maana nasema Rais Kagame sasa ananitengenezea maswali mengi sana, Kagame wasasa si wa miaka 23 iliyopita. Maisha ya Wahutu wasasa si ya miaka 23 iliyopita. Kwa lugha ya kawaida kama mchezo wa 'sinema' unavyochezwa ambapo muhusika mkuu anakuwa kulia baadaye unamkuta kushoto kwa tafsiri ya 'mtazamaji'
Kila la kheri Rwanda, Mungu ibariki Afrika, Tukutane makala ijayo kupitia https://liwale.blogspot.com/.
0654920533/0746688032/0628599961



Post a Comment

 
Top