Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais Trump ametangaza mpango wa kutangaza ushuru mpya dhidi ya China wa hadi $60bn dhidi ya bidhaa za China
China imeionya Marekani kwamba itatetea maslahi yake kuhusu biashara kulingana na chombo cha habari cha China baada ya rais Donald Trump kuwekea ushuru bidhaa za China.
Matamshi hayo yanajiri katika simu kati ya makamu wa chama tawala cha China Liu He na waziri fedha wa Marekani Steven Mnuchin. Bwana Trump ametangaza mipango ya kuziwekea ushuru wa hadi $60bn bidaa za China ikiilaumu China kwa wizi wa ubunifu.
Hatua hiyo imesababisha wasiwasi katika soko la hisa na hofu ya kuzuka kwa vita vya kibiashara. Bwana Liu ambaye ni mshauri mkuu wa maswala ya kuuchumi wa rais Xi Jinping aliambia Mnuchin kwamba Beijing iko tayari kutetea maslahi yake ya kitaifa lakini ikatumai kwamba pande zote mbili hazitakuwa na upendeleo na kufanya kazi pamoja kulingana na chombo cha habari cha Xinhua.
Wakati wa mazungumzo ya simu, ambayo yanadaiwa kuwa ya ngazi ya juu kati ya serikali hizo mbili tangu rais Trump kutangaza ushuru huo siku ya Alhamisi, bwana Liu pia aliishutumu Marekani kwa kukiuka sheria za kimataifa kufuatia uchunguzi wake kuhusu hatua ya China kuigiza utengezaji wa bidhaa zake.
Huku kukiwa na wasiwasi kuhusu biashara, mkurugenzi mkuu wa shirika la kibiashara duniani WTO Roberto Azevedo alionya kuwa vikwazo hivyo vipya vya kibiashara vitaathiri uchumi duniani. Bwana Trump hatahivyo amesema kuwa hatua ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China imeanza kuzaa matunda.
Mataifa mengine yameanza kujadiliana mikataba yenye usawa na Marekani , rais huyo alisema siku ya Ijumaa.
Kufuatia hatua hiyo ya rais Trump, China ilisema kuwa ilikua inapanga kulipiza kisasi kupitia vikwazo vya ushuru dhidi ya Marekani wa thamani ya $3bn, ikiwemo ushuru dhidi ya bidhaa za kilimo pamoja na aliminium.
Beijing imeionya Marekani kwamba haiogopi vita vya kibiashara. lakini ikasema kuwa inatumai kuzuia vikwazo hivyo kupitia majadiliano.
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Ki...Read more »
kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa...Read more »
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionHuenda ndege zikatengezwa bila madirisha katika siku za usoni.
Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua nd...Read more »
Image captionMaandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu tuhuma za ubakaji katika shule ya Moi Girls Nairobi
Walimu pamoj...Read more »
Operesheni ya mwisho ya Tundu Lissu imefanyika na kumalizika salama.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alifanyiwa op...Read more »
Haki miliki ya pichaAFPImage captionBado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi.
Bunge nchini Rwanda...Read more »
Post a Comment
aprieztmkrdezign
218168578325095
Emoticon
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.