0
Mwanajeshi wa Korea Kaskazni akikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi sita na wanajeshi wa taifa lake alipokuwa akitorokaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMwanajeshi wa Korea Kaskazni akikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi sita na wanajeshi wa taifa lake alipokuwa akitoroka
Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ambaye alipigwa risasi 6 alipokuwa akivuka mpaka wa nchi hiyo, katika harakati za kutoroka, amepata afueni na sasa anaweza kuwasiliana na wahudumu wa kimatibabu.
Madaktari wanasema kuwa wamemtaka atizame runinga na kwa sasa anaonyeshwa filamu za Korea Kaskazini.
Wiki iliyopita, askari huyo aliamua kulitoroka taifa hilo, kwa ujasiri mkubwa, ili kuingia kwenye ardhi ya taifa jirani la Korea Kusini, hatua iliyowalazimu wanajeshi wenzake kummiminia zaidi ya risasi 40, huku sita zikimpata.
Wengi walidhani amefariki, lakini kwa kudra za mwenyezi Mungu, yungali hai.
Wafanyikazi katika Hospitali hiyo wanasema kuwa japo askari huyo anahuzuni nyingi, wamemwekea bendera ya Korea Kaskazini ukutani karibu na kitanda chake, ili kumliwaza.

Post a Comment

 
Top