Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto),
akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya
ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na Mwananyamala jijini Dar es
Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za upatikanaji wa dawa na
vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa
MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Sinza, Chrispin Kayola.
Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika
picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao
mazungumzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika
picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala.
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea
wateja wa MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni
pamoja na Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo
katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu
amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na
kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30
Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi
maalumu.
Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu
walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa
wananchi.
Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema
anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na
wamedata msaada wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha
usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.
Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa
zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo
mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.
"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa ",alisema Bwanakunu.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni
asilimia 80 .
"Changamoto iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya
macho na meno ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji
tuliyonayo," alisema.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala,
Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na
MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam
Na Dotto Mwaibale - Dar es salaam
Post a Comment