Mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma ambaye ni Meneja Mkazi wa Africa
Practice mshauri akitoa shukrani zake za dhati kwa Kampuni ya Bima ya
Resolution kwa kuwakutanisha Madalali wa Bima 'Insurance Brokers' toka
sehemu tofauti nchini ambapo kwa kufanya hivyo itaongeza zaidi ufanisi
na ushirikiano baina yao na Kampuni ya Bima ya Resolution.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo
ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mambo mbalimbali kuhusiana na
kampuni hiyo na kuwashukuru madalali wa Bima kwa kwa kuungana nao katika
chakula cha usiku, pamoja na hayo alisema kuwa wapo Kenya, Uganda na
Tanzania, kwa Tanzania wapo Dar es salaam na Arusha lakini hivi karibuni
watafika Zanzibar na Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution Tanzania Bi.
Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusiana na tukio hilo la kurudisha
shukurani, ambapo pia alizitaja baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa
nipamoja na; Travel Plan, Medical plan, Liability plan,Home
Insurance,Marine insurance na Motor Private Insurance
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution Tanzania Bi.
Maryanne Mugo (aliye simama nyuma) akiwatambulisha viongozi wa Idara
mbalimbali katika kampuni ya Bima ya Resolution wa nchini Tanzania.
Bwana Melkizedech Nyau ambaye ni mtakwimu wa Bima kutoka kampuni ya Bima
ya Resolution akielezea bima ya Afya Bora kwa ajili ya watu wenye
kipato cha chini kuanzia mwaka 0 hadi 64 ambao ni kama Bodaboda, Mama
ntilie,wauza maandazi pamoja na makundi mbalimbali yanayofanana na hayo.
Alieleza kuwa ili kujiunga na Bima hiyo itakuwa vizuri watu wawe katika
kundi au Vikoba waweze kupata kwa pamoja huduma hiyo bora kutoka
kampuni ya Resolution.
Mwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku ambaye pia ni Mchekeshaji
maarufu hapa Nchini Tanzania akiendelea kutoa taratibu mbalimbali wakati
wa chakula cha usiku kilicho andaliwa na Shirika la Bima la Resulution
katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.
Mwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku akiwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na bima.
Bi. Mailda William(Kushoto) kutoka Aste Insurance Brokers ambao
walishinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution
ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya
Msichana ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima
ya Resolution
Bi. Jenifa Projest (Kulia) kutoka Aste Insurance Brokers akipewa mkono
wa pongezi kutoka kwa mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma baada ya
kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution
ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya
Salvation Army ikiwa ni
kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution
Bi. Fauzia Bairu (Kulia) kutoka Pioneer Insurance Brokers akipewa mkono
wa pongezi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution
na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati baada ya kushinda
katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi
cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Sustainable
Education ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima
ya Resolution.
Bw. Emmanuel Mkindi, Meneja wa Maendeleo ya Biashara- Biashara kwa
ujumla kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution akitoa neno la shukurani kwa
madalali wote wa bima waliofika katika tukio lao la 'Appreciation
Dinner' ambapo kaulimbiu yao inasema 'Protecting what you value' yani
tunalinda unachokithamini.
Madalali wa Bima wakiwa katika hafra ya chakula cha usiku iliyo andaliwa
na Kampuni ya Bima ya Resolution kwa ajili ya kurudisha shukurani kwa
jamii.
Post a Comment