0

           Tokeo la picha la katiba

Katiba ni sheria ama  kanuni zinazoainisha ni jinsi gani chama, kikundi au shirika litakavyojiendesha. 

Katiba ndiyo mwongozo na msingii mkuu wa shughuri zote za taasisi husika. Katiba ni kama barabara itakayo wafikisha wahusika katika malengo waliyojiwekea. Katiba lazima iwe katika mfumo wa maridhiano/makubaliano ni namna gani kikundi/chama/shirika litajiendesha kwa kufuata misingi ya haki na wajibu wa kila mwanachama.

Ili kuweza kuunda katiba ni muhimu kwa kikundi/chama/shirika kuunda kamati ndogo ambayo itashughurikia uandaaji wa rasimu ya katiba na kupeleka kwa wanachama. Kamati inaweza kushauliana na mtaalamu wa mambo ya katiba ili aweze kuwapa ushauri wa kitaalamu. Kamati ikishakamilisha rasimu ya katiba basi itapeleka katika mkutano mkuu ambapo kila kipengele kitapitiwa na wanachama watatoa maoni yao ili kuboresha katiba hiyo.

Ni muhimu hatua hizo zifwate ili kuhakikisha ushirikishwaji na uwazi katika hatua zote za uanzishaji wa katiba. Katiba ni mkataba baina ya wanachama unaoonyesha ni jinsi gani watafanya kazi kwa pamoja. Hivyo ni muhimu kila mwanachama ashiriki kwa namna moja au nyingine kuandaa katiba. Mambo muhimu yanayotakiwa kujumuishwa katika katiba ni kama yafuatayo:-

1) Ukurasa wa mwanzo (Cover page).
2) Yaliyomo
3) Tafsiri ya maneno
4) Utangulizi
5) Jina la taasisi pamoja na kifupi chake.
6) Malengo ya kuanzisha taasisi
7) Aina ya wanachama, haki zao na wajibu wao na ukomo
8) Muundo wa uongozi
9) Sifa, na wajibu wa viongozi
10) Mikutano ya taasisi na kazi zake
11) Usimamizi wa fedha
12) Chanzo cha mapato ya taasisi
13) Mwaka wa fedha wa taasisi
14) Ukomo wa taasisi
15) Majina ya waanzilishi, nafasi zao na anuani zao.

Katiba bora ni ile inaonyesha dira na uelekeo wa taasisi. Katiba bora inaonyesha picha ya taasisi kwa upana wake. Katiba kwa taasisi ni moja ya chombo cha mawasiliano ndani na nnje ya taasisi.
Kwa ushauri zaidi wa  jinsi ya kuandika katiba bora ya taasisi wasiliana nami:-

KAMA UNAHITAJI KATIBA WASILIANA NASI
Simu: 0656630250/ 0656419169/ 0689286666
Barua Pepe: mmchungulike@gmail.com  au  liwalemedia@gmail.com 

Post a Comment

 
Top