0
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga  akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mrindoko.


Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
 
Mwege wa uhuru kitaifa umeanza kutimua vumbi mkoani Kigoma kwa kuibua miradi lukuki iliyojengwa chini ya kiwango katika halmashauri ya wilaya ya uvinza huku kukiwa na hofu ya ufujaji wa fedha za umma katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Kufuatia hali hiyo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017 Amour Amour amekataa kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo mitano inayohusisha ujezi wa nyumba za walimu vyumba vya madarasa na hofisi mbalimbali na kuagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo
 
Aidha Kiongozi huyo ametoa muda wa siku tatu kwa muhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza na mkandarasi aliyejenga mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Nguruka iliyopo katika kata ya nguruka kurekebisha baadhi ya kasoro zilizobainika katika mradi huo kwa kutumia fedha zao .

Maagizo hayo aliyatoa jana mara baada ya kuanza kukagua na Kuzindua Miradi sita ya halmashauri hiyo katika Shule ya Sekondari Nguruka, ambapo katika mradi wa Nyumba za shule hiyo walibaini kuwepo na nyufa katika majengo hayo na matumizi yafedha nyingi katika kukamilika kwa Mradi huo na kumuagiza mkurugenzi kuwasimamia muhandisi wa halmashauri na Mkandarasi wa mradi kufanya marekebisho ndani ya siku tatu na kupelekewa taarifa ya marekebisho hayo.

Hata hivyo Kiongozi huyo aliahirisha zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kijiji cha Malagalasi kata ya Nguluka Wilayani uvinza mkoani kigoma kufuatia jengo hilo kujengwa chini ya kiwango.

Pia Amour aliwaagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuchunguza mradi huo kama kuna vitendo vya rushwa vilifanyika, kutokana na mkandarasi huyo alieshindwa kufanyia marekebisho, mapungufu ya awali ambapo baada ya Mkandarasi mwingine kukabidhiwa mradi huo bado mapungufu yaliendelea kuwepo katika mradi.

Amour alisema atahitaji apatiwe taarifa ya marekebisho hayo baada ya siku tatu na taarifa hiyo ataifikisha mahari usika, pia alisema hawawezi kuvumilia fedha za serikali ziendelee kuibiwa kwa kutekeleza miradi mibovu isiyo na viwango ni lazima miradi yote inayotekelezwa ya Maendeleo iwe imara na inayodumu kwa muda mrefu kutokana na fedha wanazozitoa.

" sisi tumekuja kufanya kazi hatuta kubali kuzindua wala kupokea taarifa ya miradi mobov, ninaomba marekebisho haya yafanyike haraka sana na kabla hatujaenda Mkoa mwingine hii taarifa niipate na niifikishe sehemu husika hatuwezi kuvumilia mapungufu haya yaendele katika halmashauri zetu nilazima muwe na uangalizi na usimamizi mzuri wa miradi ilikuhakikisha tunapata miradi iliyo imara",alisema Amour.

Alisema Miradi ya Nyumba za Walimu imetofautiana hata katika fedha kutokana na uzembe wa usimamizi wa Miradi kwa halmashauri, Wakandarasi wana Lugha nzuri za kuwadanganya Wakurugenzi na Wasimamizi ilikulinda vibarua vyao, kupasuka kwa Nyufa za Nyumba inatokana na uzembe wa Mkandarasi na usimamizi Mbovu wa halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenz wa halmashauri, Weja Ng'olo alisema Mradi huo ulighalimu zaidi ya milioni 162 hadi kukamilika, na wao kama Halmashauri walitembelea mradi huo na kubaini baadhi ya Mapungufu ambapo walimuomba Mkandarasi kuyafanyia marekebisho na aliposhindwa waliamua kumpa kazi hiyo mkandarasi mwingine.

Alisema marekebisho hayo watayafanya kwa kutumia fedha ya Mkandalasi aliyobaki anaidai halmashauri hiyo ilikuhakikisha Mapungufu yote yaliyokatika Mradi yanamalizika na kuendlea kutumiwa na Walimu na familia zao.

Post a Comment

 
Top