Rashid makolelo akipokea Kadi ya Bajaji aliyosaidiwa na mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mh. KASSIM.MAJALIWA.Mwonekano wa Bajaji aliyokabidhiwa Bw. Rashid makolelo
Na. Abdulaziz, Lindi
Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ambae pia ni Waziri mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa amekabidhi chombo cha usafiri wa bajaj kwa bw Rashid Makolelo ambae ni mlemavu wa miguu ili kumsaidia kurahisha ujasilimali wake.
Akikabidhi Bajaj hiyo kwa Bw Rashid Makolelo mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa kijiji cha Mmawa Kata ya Nkowe wilayani humo kwa niaba ya mbunge wajimbo hilo, Katibu tawala wilaya ya Ruangwa, Twaha Mpembenwe amesema pamoja na majukumu ya Kitaifa mbunge wa jimbo hilo ataendelea kushirikiana na jamii ikiwemo kutoa misaada mbalimbali.
Aidha Twaha alieleza kuwa kutolewa kwa msaada huo ni chachu kwa mlemavu huyo kuongeza jitihada za ujenzi wa Taifa ikiwa pamoja na kujitafutia kipato.
Awali Katibu wa mbunge jimboni, Kasambe Hokororo akikabidhi bajaj hiyo ikabidhiwe kwa mlengwa amewahaidi wakazi wa jimbo hilo kumuombea na kumpa ushirikiano mbunge wao kutokana na kuwa mtendaji mkuu wa serikali na ataendelea kuwasaidia kadri apatavyo nafasi bila kujali Itikadi za siasa kwa wananchi wake.
Nae Bw Rashid Makolelo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo hakusita kutoa shukrani kwa mbunge huyo kwa kumsaidia usafiri utakaomuwezesha kuongeza tija katika biashara yake huku ikirahisha huduma mbalimbali za kifamilia.
Pamoja na msaada huo pia mlemavu mwingine anaejulikana kwa jina la Sikonde nae amekabidhiwa msaada wa pikipiki kwa ajili ya kumuingizia kipato huku ikibainika kuwa Rashid makolelo pamoja na ulemavu alionao ujishughulisha na kilimo cha bustani kwa mazao ya vitunguu na nyanya ambazo soko lale la mauzo ni mkoani Mtwara.
Post a Comment