0

Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
KATIKA kuhakikisha wilaya ya Nachingwea haigeuki na kuwa kichaka cha wahalifu. Mkuu wa wilaya hiyo, Rukia Muwango amepiga marufuku usafirishaji wa abiria kwa pikipiki (bodaboda) kufanyika zaidi ya saa sita usiku.
Muwango alitoa tangazo hilo jana katika kijiji  cha Mpiruka wilayani humo alipokuwa anazungumza na wananchi wa kata ya Mpiruka kupitia mkutano wa Hadhara. Muwango ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hii, alisema kutokana na matukio ya kiusalama yanayojitokeza katika mkoa wa Pwani, nidhahiri kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara haipo salama sana.
Kwakuzingatia ukweli huo ameamua kuchukua hatua za makusudi ili wahalifu wasipate nafasi ya kujipenyeza na kuingia wilayani humu. Licha ya usafiri wa bodaboda, lakini pia amewaagiza wamiliki wa nyumba za kulala wageni wahakikishe wanawalaza watu wenye vitambulisho au barua za utambulisho zinazotoka kwenye serikali za vijiji au mitaa.
“Tumesha zungumza na wasafirishaji wa mabasi wahakikishe wanawakatia tiketi watu wenye vitambulisho,” alisema Muwango.
Alibainisha kuwa baadhi ya wahalifu wanatumia usafiri wa mabasi hata hivyo wanapofika katika maeneo ambayo sio makazi ya watu wanaomba hudhuru washuke ili wakajisaidie porini. Hata hivyo hutokomea moja kwa moja.
Aidha Muwango aliwaasa wananchi kuwafuatilia na kuwa baini watu wasiowatambua wanaoingia katika maeneo yao. Katika hatua nyingine mkuu huyo aliwaasa wananchi kuibua miradi ya maendelo nakuanza kuitekeleza ili serikali isaidie kukamilisha. Ikiwamo ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma, vyumba vya madarasa, na zahanati. Badala ya kusubiri serikali ifanye mambo yote.

Post a Comment

 
Top