WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imebainisha kuwa mpaka sasa haitambui
na wala haina uthibitisho sahihi kuhusu wananchi wa Zanzibar
waliofanyiwa ukatili, kunyanyaswa, kupigwa ikiwemo kunyang’anywa mali
zao na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama inavyodaiwa.
Aidha, imewataka wenye uthibitisho kamili wa matukio hayo, kuwasilisha malalamiko yao kwa wizara hiyo husika kwa ajili ya uchunguzi na hatua kamili kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Akijibu swali la Mbunge wa Bumbwini, Mohamed Amour Mohamed (CUF), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamad Yusuf Masauni alisema mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyoripotiwa kwenye vituo vya Polisi visiwani Zanzibar kuhusu uhalifu huo.
Katika swali la msingi na nyongeza, Mohamed alitaka kujua serikali ina kauli gani kutokana na matendo ya unyanyasaji, kupigwa na kunyang’anywa mali zao dhidi ya wananchi yanayofanywa na vikosi vya SMZ.
Katika swali la Mbunge wa Malindi, Ally Saleh Ally (CUF), alitaka kujua kama kuna uwezekano wa serikali kuunda tume maalumu kwa ajili ya kuchunguza matukio hayo ya uhalifu dhidi ya wananchi ambayo yamekuwa yakiripotiwa bila hatua stahiki kuchukuliwa kwa wahusika.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema alibainisha kuwa serikali imekuwa ikifanyia kazi hoja zinazowasilishwa kwa utaratibu unaotambulika ulio rasmi.

Post a Comment