Ofisa Usajili Msaidizi wa Rita, Jane Barongo amesema jana alipokuwa akizungumza na HabariLeo kuhusu nakala hizo za vyeti ambazo kwa asilimia kubwa zimekuwa hazirudishwi hivyo kufanya kazi ya uhakiki wa vyeti vya ndoa kuwa ngumu.
Amesema kutokana na ugumu huo wa kurudisha nakala hizo, Rita imeandika barua kwa taasisi za kidini na wasajili wote wa ndoa kuhusu kurudisha nakala hizo za ndoa zilizofungwa.
“Changamoto ni kwamba sio wote wanaopeleka hizo nakala hivyo inawawia vigumu wakati wa kuthibitisha cheti,” alieleza Barongo.
Pia alisisitiza kuwa katika uhakiki uhalali wa vyeti vya ndoa, Msajili Mkuu wa Ndoa anahakiki vyeti vya serikali tu, kwani kuna baadhi ya taasisi za kidini vinatoa vyeti vyao hali inayowafanya wanandoa kutopata haki zao.
Aliitaja mikoa iliyoitikia kuanza kurudisha nakala hizo kuwa ni Arusha, Mtwara, Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma.
Alisisitiza kuwa katika kuhakiki cheti, Rita ndiyo inayotoa vyeti vya serikali vya ndoa zote za serikali, kidini na kimila hivyo inapotokea suala la kujua uhalali wa cheti hicho, wakala hao ndiyo ina mamlaka.
Post a Comment