0



BAADA ya timu yake kufanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumapili iliyopita kwa kuwaondoa watani zao Simba, kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, amesema kwamba itakuwa ngumu wao kuondoka kwenye nafasi hiyo.
Kamusoko alisema kuwa uwezo na malengo ambayo walikuwa wamejiwekea yametimia na sasa wanachohitaji ni kulinda wasiondoke kwenye nafasi hiyo.
"Asante Mungu kwa kupata pointi tatu muhimu, na sasa tunaongoza ligi, natumaini kwa neema na baraka za Mungu, tutaendelea kupambana kwa ajili ya kuongoza mpaka mwisho wa msimu," alisema kiungo huyo raia wa Zimbabwe.
Aliongeza kuwa kila mechi wanayocheza tangu msimu ulipoanza ni ngumu kwa sababu hakuna timu inayokubali kupoteza mchezo kirahisi huku akisema kuwa timu zote ni sawa.
Yanga imekaa kwenye uongozi wa ligi ikiwa na pointi 46 baada ya mechi 20 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 45 na Azam FC wenye pointi 34 katika nafasi ya tatu.

Post a Comment

 
Top