Agizo
la Rais wa jamhuri ya muungano wa Dkt. John Pombe Magufuli la kulitaka
jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung'oa matairi vyombo
vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka
la tekelezwa kwa vitendo ambapo takribani pikipiki kumi na sita
zimeng'olewa matairi na wahusika wakitarajiwa kufikishwa mahakamani hapo
tarehe 2 febuari mwaka huu.
Agizo
hilo la rais Magufuli alililoa kwa mara ya pili katika shughuli ya
uzinduzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka lengo likiwa ni kuhakikisha
miundombinu ya mradi huo haziharibiwi ambapo kamanda wa jeshi la polisi
kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga amesema zoezi hilo
ni mwanzo tu na yeyote atakayetumia miundombinu hiyo hataonewa huruma.
Awadhi
Haji ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani katika jiji la Dar es
Salaam ambapo licha ya kukiri idadi kubwa ya waendesha bodaboda wamekuwa
wakipita katika barabara hizo ameendelea kuwaasa watumiji wa vyombo vya
moto kutambua miundombinu ya mradi huo ni kwa manufaa ya kila mtanzania
hivyo kuna kila sababu ya kutunzwa na kila mtu.
Watuhumiwa
wa makosa hayo na mengine ya uvunjifu wa sheria za barabarani pamoja na
abiria wao wakiwa takribani sitini na moja baadhi ya waliozungumza na
ITV licha ya kutokuwa na sababu za msingi za kutumia barabara hizo
wamewahadharisha wenzao kwa kuwa adhabu iliyotajwa na Mh rais ni kweli
inatekelezwa.
Watuhumiwa wote wakiwemo abiria wao wataendelea kukaa rumande hadi febuari 2 mwaka huu watakapofikishwa mahakani.
Chanzo: ITV
Chanzo: ITV

Post a Comment