Na. Ahmad Mmow, Kilwa
Mkuu
wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesitisha uhamisho wa watumishi wa nne
kati ya watano waliotakiwa kuhama kutoka kwenye kituo cha afya cha
Tingi wilaya ya Kilwa.
Zambi
alisitisha uhamisho huo juzi alipokuwa anazungumza na wananchi wa kata
ya Tingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Tingi.
Mkuu
huyo wa mkoa ambae kabla ya kutoa uamuzi huo alisikiliza maelezo ya
wananchi, baadhi ya waguuzi, mganga kiongozi wa kituo hicho na baadhi ya
wakuu wa idara wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Alisema
kutokana na utata wasababu zilizoelezwa kuhusu uhamisho huo na
mazingira yaliyosababisha kifo cha mtoto wa miaka tisa aliyefia katika
kituo hicho mwanzoni mwa mwezi uliopita, aliamua kusitisha uhamisho wa
watumishi wanne kati ya watano waliopewa barua za uhamisho hadi
yapatikane matokeo ya uchunguzi utakaofanywa na tume maalumu itayoundwa
na ofisi yake hivi karibuni.
Alisema
pamoja sababu zilizotolewa na mganga mkuu wa hosipitali ya wilaya ya
Kilwa, Dkt Vitalis Katalyeba kuhusu uhamisho huo lakini ameona kuna haja
ya kusitisha ili uchunguzi wa kina ufanyike.
"Pamoja
na sababu zilizo elezwa lakini bado uchunguzi unahitajika, kituo hiki
kina watumishi 22 sawa na kituo cha Masoko ambacho kipo karibu na
hosipitali ya wilaya, kinahudumia watu wengi kuliko kituo cha Masoko.
Lakini wamehamishwa watumishi watano wakati Masoko wamehamishwa wawili
tu, hata hivyo uhamisho unafanyika kukiwa ni muda mfupi tangu kuibuliwa
tatizo la umeme na yanayotokea baada ya kuelezwa tatizo hilo, wananchi
hawa nirahisi kuamini kuwa umetokana na sababu hiyo," alisema Zambi.
Kuhusu
mazingira ya kifo cha mtoto, mkuu wa mkoa Zambi alisema kuna utata
mkubwa wamaelezo uliosababisha kuhitajika uchunguzi wa kina.
Alibainisha kwamba japokuwa maelezo ya mlezi wa mtoto aliyefariki,
Magreth Nguli, kwakiasi kikubwa yalifafana na ya muuguzi Mwanaisha
Amanzi kuhusu muda aliofariki mtoto huyo, muda ambao alifikishwa katika
kituo hicho kutoka katika zahanati ya Miteja, muda muuguzi Mwanaisha
aliomba gari kwa mganga mkuu wa wilaya kwa ajili ya kumkimbiza
hosipitali na muda ambao gari hiyo ilifika katika kituo hicho wakati
mtoto huyo amefariki.
Lakini
maelezo ya mganga mkuu yalitofautiana na maelezo ya Mwanaisha na
Magreth. Huku baadhi ya fomu za taarifa zilizoandikwa kituoni hapo
zikiwa zimebadilishwa maelezo ya taarifa zikiwa na miandiko ya watu
zaidi ya wawili.
Sambamba
na uamuzi wa kusitisha uhamisho huo, Zambi ambae pia nimwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, alimvua madaraka mganga kiongozi wa
kituo hicho, ofisa tabibu Christopher Kunde. Huku akimuagiza mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Zabron Bugingo ambae alikuwepo
mkutanoni hapo, amuhamishe kutoka katika kituo hicho.
Kutokana
na kuchelewa kuandaa taarifa muhimu za kifo cha mtoto huyo kwa
takribani majuma mawili tangu kutokea kifo hicho. Tena ni baada ya mkuu
wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai kwenda kituoni hapo na kuelezwa
kuwa pamoja na sababu nyingine kifo cha mtoto huyo kilichangiwa na
kitendo cha kutopelekwa gari haraka.
Awali
muuguzi Mwanaisha ambae kwakiasi kikubwa maelezo yake yaliungwa mkono
na mlezi wa mtoto huyo alisema mtoto huyo alifikishwa kituoni hapo saa
nne asubuhi na ndio muda ambao alimpigia simu mganga mkuu wa wilaya
kumuomba gari hata hivyo hakupata ushirikiano kutokana na kilichoelezwa
kutokuwa na mahusiano mazuri baina yao.
"Nilimpigia
simu saa kwenye saa nne, badala ya kumuambia alisema mimi sikupaswa
kumuomba. Bali muuguzi wa zahanati ya Miteja huku akinilaumu kwanini
nilimueleza mkuu wa wilaya na waandishi wa habari tatizo la umeme."
aliniuliza mgonjwa alikuwa na umri gani nilipomtajia alikata simu na
kuacha kabisa kupokea simu nilizokuwa na mpigia hadi nilipotumia simu ya
mmoja wa ndugu za mgonjwa," Alisema Mwanaisha.
Kwa
upande wake dkt Katalyeba ambae maelezo yake kuhusu sababu za uhamisho
wa wawatumishi hao yaliungwa mkono na katibu wa bodi ya afya ya
hosipitali ya wilaya, John Maongezi. Alisema uhamisho huo ulikuwa wa
kawaida kutokana na upungufu mkubwa watumishi wa idara ya afya wilayani
humo, kiasi cha kusababisha baadhi ya zahanati kuwa na muuguzi mmoja.
"Uhamisho
huu haujalenga kituo cha Tingi pekee yake bali hata vituo vingine
watumishi wake wamehamishwa na hakuna sababu nyingine zaidi ya hiyo," alisema Dr Katalyeba.
Kuhusu kuchelewa kupelekwa gari na muda gari hiyo ilipofika katika kituo cha Tingi. Mganga mkuu huyo alisema "Taarifa
ilinifikia saa sita na nusu, aliyenipigia simkumbuki maana nilikuwa
naendelea nakazi ya upasuaji, hata simu niliwekewa sikoni na mtu, na
gari hiyo ilifika saa nane na nusu mchana katika kituo hiki," alisema Dr Katelyeba.
Mwanzoni
wa mwezi uliopita, mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai alikwenda
katika katika kituo hicho nakuambiwa kuwepo changamoto ya umeme na
maji.
Ambapo
pia alikwenda mwishoni mwa mwezi kuona utekelezaji wa agizo lake kwa
shirika la umeme (TANESCO) kuhusu kushugulikia tatizo la umeme katika
kituo hicho.
Ndipo
alipoelezwa kuwa pamoja na tatizo la umeme kushugulikiwa kikamilifu na
kumalizwa. Lakini ziara yake na maagizo aliyotoa yalisababisha kujenga
uhasama baina ya muelezaji wa tatizo hilo la umeme (Mwanaisha Amanzi) na
mganga mkuu wa hosipitali ya wilaya (Dr Vitalis Katalyeba).
Post a Comment