0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameshiriki zoezi la kuteketeza silaha haramu 5,608 zilizokamatwa kwenye matukio ya kihalifu na zingine kusalimishwa hapa nchini.

Silaha haramu zikiwa zimepangwa katika uwanja wa Lake Tanganyika tayari kwa uteketezaji wakati wa zoezi hilo lililofanyika mkoani kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu
Waziri Nchemba ameandika katika ukurasa wake wa Instagram, “Tanzania hatuungi mkono wa umiliki wa silaha haramu.Hapa tukiteketeza silaha haramu.” Aidha aliwaomba wananchi kuendelea kuliunga mkono jeshi la polisi. “Tuendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi letu kufichua watu wanaomiliki silaha isivyo kihalali”.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akiangalia silaha aina ya SMG iliyotengenezwa kienyeji ambayo ni mojawapo ya Silaha zilizoteketezwa wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha haramu lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akikagua silaha haramu zilizoandaliwa kwa ajili ya kuteketezwa wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha hizo lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akizungumza na wakazi wa mkoa wa kigoma waliojitokeza kushuhudia zoezi la la kuteketeza Silaha haramu lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali kupambana na uhalifu hapa nchini

Silaha haramu zikiwaka moto wakati wa zoezi la kuteketeza Silaha haramu lililofanyika mkoani kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu
Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Post a Comment

 
Top