0
Viongozi  wa  vyama  vya  siasa  wametakiwa  kushirikiana  na  kuondoa  chuki pamoja na fitna ili kuleta maendeleo nchini.

Rai hiyo imekuja baada ya wajumbe wa kikao  cha halmashauri  kuu ya CCM mkoa wa magharibi kichama   kukutana  katika   ukumbi  wa  hoteli ya ngalawa iliyopo  bububuu kihinani  kujadiliana  masuala  mbaimbali  juu  ya  utendaji  kazi  kwa mwaka unaomalizika 2016 na unaoanza 2017.

Balozi Seif Ally Iddi makamo wa pili wa Raisi Zanziba na mlezi wa chama cha Mapinduzi Zanzibar

        Akizungumza  katika  kikao  hicho   mlezi wa chama  cha mapinduzi CCM  Zanzibar   Balozi  Seif  Ali  Iddi ambae pia ni makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar  amesema  kuwa  ni  vyema  kuondoa  chuki  katika  utendaji  wa  kazi  na  kukaa  kwa  pamoja  kufanya  kazi  kwa  umakini  ili  kusogeza  maendeleo  mbele.

Nae   mkuu  wa  mkoa  mjini  magharibi  Ayoub  Mohammed  Mahmoud  amesema  kuwa    baadhi  ya  masheha  wamekuwa   na  tabia  ya  kushiriki  katika  kuuza  viwanja  katika  maeneo  ya  mabonde  hali  ambayo  ni  hatarishi  kwa  wananchi na kusema kuwa atakae kundulikana kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa juu yake.

Post a Comment

 
Top