Kuna mambo mengi sana kwenye ili jambo, ila kwa uchache naweza
kusema katika mazungumzo yanayopendwa basi mazungumzo ya ngono au
kuridhishana kimapenzi baina ya jinsia mbili ndio yanaongoza sana,
wengine huita Hot Night
Kwa kweli ili ni janga kubwa sana kwa vijana au niseme watu wengi wenye
kushiriki mijadala kwenye mitandao na haswa makundi (groups) zenye
michanganyiko ya kijinsia.
Ukizunguka kwenye mitandao ya Kijamii, habari nyingi zinazojadiliwa na
vijana ni mahusiano ya Kijinsia (Kingono). Na ufikia mpaka kuambiana ni
jinsi gani unaweza mfanyia mwenzio hivi au vile mpaka akaridhika.
Maswala ya simulizi za Ngono kwa Kisingizio cha Kuimarisha Ndoa za watu
au mahusiano yamekuwa ni gumzo kubwa sana na kufikia mahali hata mtu
akisema kuwa haya maswala si vema kuyaweka kwenye mijadala hii ya wazi,
utaonekana kuwa wewe umepitwa na wakati au mshamba.
Ili limekuwa ni tatizo moja kubwa sana na kwa bahati mbaya sana limewakumba hata wale wenye kujionyesha kuwa wameshika dini.
Waislamu nao hawakubakia nyuma wameiga mazungumzo hayo na kuyapa majina
kadhaa wa kadha tena wakiambatanisha na Hadith za Mtume (saw), kwa lengo
la kuhalalisha kile ambacho kimeharamishwa.
Kuzungumzia Maswala ya ngono na namna ambavyo unaweza kumstarehesha
Mke/Mume kwa kuandika kila jambo hatua kwa hatua na kutaja viuongo
husika kwa majina yake halisi ni sawa na kuangalia picha za uchi au
picha chafu za Ngono.
Katika Imani ya Kiislamu ni haramu kwa Muislamu kusoma au kutazama filamu za ngono ambazo kwayo huamsha hisia na ashiki.
Kwa sababu zozote zile haifai katika Uislamu. Hili hata kimantiki
haliingii akilini kwani wale ambao utakuwa ukiwasoma au kuwaangalia
watakuwa katika hali ya uchi ambayo imekatazwa na Uislamu.
Simulizi hizi ujenga taswira
kwenye ubongo wa msomaji na kuchochea zile kemikali zenye kuamsha hisia
za kufanya jimai na zinamtia Muislamu hawaa na ashki ya bure na hivyo
kumkaribisha yeye na zinaa.
Utakuta mtu anajionyesha kama ustadhi/ustaadha mzuri, lakini linapokuja
swala kama ili ndio uwa mstari wa mbele kutetea na kushadidia kuwa
inafaa kwa sababu itaimarisha ndoa na kuwafunda wale wenye kutarajia
kuingia kwenye ndoa.
Tena uona sifa kubwa kwa kule kubandika maswala ya ngono na kujionyesha
kuwa yeye ni mahiri sana na mwenye ujuzi wa maswala hayo.
Haya ni matokeo ya kuzarau mafunzo ambayo zamani wazazi wetu waliweza
kuwakusanya vijana balekh na kuwapatia mafunzo tena kwa siri na haswa
wale waliotarajiwa kuingia kwenye ndoa na kuwafahamisha kinaga ubaga
nini kinapaswa kufanywa kwenye ndoa na yapi hayafai.
Tulipoanza kuyazarau mafunze yale kwa kisingizio kuwa yamepitwa na
wakati, matokeo yake ni kuwepo uwanja huru mwenye kila lake kulirembea
kwenye mtandao, bila kuzingatia maadili ya kijamii, dini wala kabila.
Hii naweza kusema ni sawa na kufundisha uchawi kisha ukawaambia wanafunzi wako wasiwaroge watu kwa kuwa si jambo zuri.
Matokeo yake ni hodi zisizokwisha kwenye inbox, wataanza na salamu na
kuelezeana matatizo ya hapa na pale. Watajifanya kuombeana madua na
maneno mazuri mazuri.
Siku ya pili utapigiwa simu na mazungumzo yataendelea na kupelekea
kuombana picha na matokeo yake ni kupeana ahadi za kukutana na mwishowe
ni kungonoana.
Waislam, tumewacha mafundisho ya dini na kila mtu siku hizi amekuwa ni ulamaa mwenye kutoa fatawa na wajuzi wa fiqh, ule utaratibu na nidhamu ya kukaa chini ya Masheikh imepitwa na wakati na siku hizi Ulamaa mkubwa mwenye kutegemewa ni Sheikh Gugol Ibn Intanetii.
Waislam, tumewacha mafundisho ya dini na kila mtu siku hizi amekuwa ni ulamaa mwenye kutoa fatawa na wajuzi wa fiqh, ule utaratibu na nidhamu ya kukaa chini ya Masheikh imepitwa na wakati na siku hizi Ulamaa mkubwa mwenye kutegemewa ni Sheikh Gugol Ibn Intanetii.
Tunamuomba Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atusamehe kwa makosa yetu mbali mbali tunayofanya mchana na usiku.
Post a Comment