0
Bodi ya chakula na vipodozi Zanzibar imekanusha taarifa zilizoenea kuwa imethibitisha matumizi ya vipodozi aina ya karolaiti kwa matumizi ya binadamu.
Mkuu wa biashara na uwendeshaji kutoka bodi ya chakula na vipodozi Zanzibar  Abdul-Aziz Shaib akizungumza na waandishi wa habari

          Akizungumza na kituo kimoja cha redio visiwani Zanzibar , mkuu wa biashara na uwendeshaji kutoka bodi hiyo Abdul-aziz Shaib amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa matumizi ya vipodozi hivyo ni hatari kwa matumizi ya afya ya binadamu.
          Aidha ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaoendelea kuuza bidhaa hiyo na kusema Serikali haitosita kuwachukulia hatua za kisheria kwa watakaobainika.

          Pamoja na hayo Abdul-aziz ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika pindi wanapobaini duka linalouza vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.

Post a Comment

 
Top