0
Michuano ya Mapinduzi Cup inayofanyika kila mwaka visiwani Zanzibara inatarajiwa kuanza rasmi  leo tarehe 30 mwezi 12 saa 2:15  usiku katika uwanja wa amani kwa kuzikutanisha timu kati ya TAIFA YA JAN’GOMBE  dhidi ya timu ya JAN’GOMBE BOYS  zote za hapa Zanzibar

michuano hiyo inayoanza kutimua vumbi hii leo imeshirikisha timu tisa( 9) ,tano kutoka Zanzibar ikiwemo KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys na Jamuhuri  ambazo ndio wenyeji wa michuano hiyo.
Timu tatu kutoka Tanzania bara ambazo ni Azam,Yanga na Simba huku moja kutoka Uganda URA ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya mapinduzi kwa mwaka 2016 .
michuano hiyo ya Mapinduzi Cup inayoanza hii leo Desember 30 mwaka 2016  inatarajiwa kufika tamati January 13 mwak 2017
Mapinduzi cup huchezwa kwa mfumo wa makundi ambapo Timu zote tisa shiriki zimegawanywa katika makundi mawili  na yanga anaonekana kuwa kundi B, akiwemo  na AZAM . huku vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba wao wapo katika kundi A ambapo wapo na bingwa mtetezi URA kutoka UGANDA.
,,
Angalia hapo chini nimekuwekea makundi pamoja na ratiba

MAKUNDI MAPINDUZI CUP

 KUNDI A : Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
 KUNDI B : Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.


RATIBA  YA MAPINDUZI CUP .2016-2017
 30/12/2016 Taifa ya jang'ombe vs Jang'ombe boys saa 2:30 usiku.
 1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang'ombe saa 2:30 usiku.
 2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri,Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
 3/1/2017 Jang'ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri,KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
 4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
 5/1/2017 KVZ vs Jang'ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.

6/1/2017 Taifa ya jang'ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
 7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
 8/1/2017 Simba vs Jang'ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang'ombe vs URA 2:30 usiku.
 10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainal ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainal ya pili.

13/1/2017 FAINAL saa 2: 30 usiku.

Post a Comment

 
Top