INASIKITISHA
SANA: Binti mmoja ambaye ni model na mwimbaji wa muziki aliyetambulika
kwa jina la JULIANA ISAWAFO (pichani) ambaye picha yake ilisambaa kwenye
mitandao ya kijamii kuanzia jana ikionyesha mwili wake ukiwa umetupwa
eneo la Ndoro nje kidogo ya Chuo Kikuu cha Makumira, Arusha baada ya
kudaiwa kubakwa na watu wasiojulikana.juliana-1
julianaMmoja
wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake
halikufahamika mara moja) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na
kusema kuwa ameokotwa majira ya saa tano asubuhi jana akiwa amekufa na
mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mpunga nje kidogo ya eneo la
chuo hicho.
Mbali
na kuthibitisha kifo hicho, kiongozi huyo ameeleza pia kuwa, msichana
huyo ni mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila hakuwa mwanafunzi rasmi
kama watu wanavyodai. juliana-2 Ameongeza pia kuwa, msichana huyo
alikuwa akiishi ndani ya eneo la chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja
wa walimu wa Sanaa chuoni hapo.
Mwisho
akaeleza hisia zake namna ambavyo familia ya chuo hicho ilivyoguswa na
msiba huo kwani msichana huyo alikuwa kama dancer wa matamasha
mbalimbali ya Chuo cha Makumira.
Audio: Sikiliza Mahojiano | Msichana Abakwa Hadi Kufa Makumira University, Arusha
Post a Comment