Wanawake hawa, wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 96, walipiga kura kwa njia ya posta na kupashana habari
Tarehe 8 Novemba,
mamilioni ya wanawake wa kimarekani watafanya kile ambacho hawakupata
fursa ya kukifanya kabla - kumpigia kura mwanamke aliyeteuliwa kama
mgombea mkuu wa chama kuwa rais wa Marekani.
Kwa baadhi yao hii kikomo cha miaka 96 ya kusubiri.
Yeyote aliyezaliwa kabla ya tarehe 18 Augusti 1920 nchini Marekani
alianza maisha katika nchi ambayo haikumruhusu wanawake kupiga kura.
Hao
ni pamoja na Estelle Schultz, mwenye umri wa miaka 98, aliyekuwa
akifanya kazi kwenye viwanda viwili katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia
na mwalimu wa muda mrefu,ambaye alipelekwa kwenye kituo cha kupigia kura
kama mtoto na mama yake kushuhudia namna kura zinavyopigwa.
Estelle
ana matatizo makubwa ya moyo na yuko chini ya uangalizi wa hospitali.
Lakini anasema: "nimeamua kwamba ningependa kuishi muda mrefu wa
kutosha kuweza kushudia kuchaguliwa kwa mwanamke wetu wa kwanza rais ."
Mwezi Oktoba, alipokuwa akipiga kura yake ya awali
kwa njia ya posta, alisema kuwa alibaini ni kiwango gani hali hiyo
"ilivyo muathiri" , na akamuomba mjukuu wake wa kike Sarah kutuma
picha yake hii kwenye Facebook
Picha hii ilipendwa na mamia ya
watu kwa ishara ya ''like'', suala lililoibua shauku ya sara na familia
yake kutafuta taarifa zinazofanana na ya bibi yao.
Waliwapata
wengine wengi, na wavuti " Nilisubiri miaka 96 " ulianzishwa, na kujaa
kauli kutoka kwa wafuasi wa Hillary Clinton waliozaliwa kabla wanawake
kuwa na haki ya kupiga kura.
Baadhi ni watu wazima wa kutosha
kiasi cha kukumbuka wakati wanawake walipopewa fursa ya kupiga kura,
mara baada ya kuidhinishwa kwa marekebisho ya 19 ya katiba ya Marekani.
"nakumbuka nikimsindikiza mama yangu tukiwa kwenye
farasi kuelekea kwenye kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa kwanza
ambapo wanawake waliruhusiwa kupiga kura. Hatimae baada ya muda mrefu
nilikuwa na haki ya kupiga kura ,"aliandika Juliet Bernstein mwenye
umri wa miaka 103 kutoka Massachusetts, ambaye alizaliwa mwaka 1913,
na kupaya shahada ya kwanza kwa kutiwa hamasa na mama yake.
Mama yangu alikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kukata nywele zao
kuwa fupi na kubadilisha mtindo wa sketi ndefu zilizokuwa zikiburuzwa
kwenye matope na kuvaa magauni mafupi ," alisema Beatrice Lumpkin,
mwenye miaka 98, kutoka Chicago.
"yote ni juu ya haki zetu ,
wakianza na haki yao ya kupiga kura. Nilipokuwa mtu mzima kiasi cha
kuelewa ni vipi wapigania haki ya kupiga kura nilijivunia sana''
Baadhi ya wachangiaji wa mtandao huo wanasema wanayo furaha kuwa na
fursa ya kumpigia kura mwanamke kama raia katika kipindi cha uhai wao -
kitu ambacho wengi hawakudhani kingewezekana.
Post a Comment