Meya wa jimbo la
Minneapolis ameitetea jamii ya Wasomali nchini humo baada ya mgombea wa
Republican Donald Trump kuwashtumu kwa kueneza itikadi kali.
Betsy Hodges amesema kuwa wahamiaji wa Somali wameufanya mji wake katika jimbo la Minnesota kuwa Imara zaidi.
Katika ukurasa wake wa facebook alimwambia Trump:
''Unasema kuwa tusikubali kivuruga jamii zetu kama ambaye tayari ushaanzisha jimbo la kibepari unavyopanga kuligeuza taifa hili.
Hii
ni Marekani,Donald na raia wa Somalia katika maeneo ya Minnesota na
Minneapolis hawazivurugi jamii zetu,badala yake wanazidi kuziimarisha.
Kila
kitu ulichofanya kuanzia biashara zako na unyanyasaji wako wa kijinsia
mbali na chuki zako dhidi ya Uislamu na kuwalaumu wengine kwa matatizo
uliozua mwenyewe-kuna saliti ujinga wako wewe mwenyewe.
Lakini ni
maadili ya Minnesota na tutayaunga mkono siku ya Jumanne.Minneapolis
imeimarika kwa sababu ya Wasomali pamoja na wahamiaji wa Afrika
mashariki na wakimbizi ndani yake.
Ni heshima kubwa kwangu kuwa Meya wa mji ulio na idadi kubwa ya Wasomali nchini Marekani''.
Post a Comment