MKUU WA MKOA LINDI GODFRAY ZAMBI AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MAVUJI WILAYANI KILWA MKOANI LINDI
Wananchi wa kijiji
cha Mavuji wilaya
Kilwa Mkoani Lindi wameuomba
uongozi wa mkoa huo kusimamia
kurudishwa kwa maeneo
yao zaidi ya hekta elfu 20
ziliyochukuliwa na wawekezaji
ambalo halijafanyiwa kazi ili kusudiwa.
Malalamiko hayo yametolewa
na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara wa
mkuuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi
ambaye alikuwa moja ya ziara yake
wilaya humo kuhimiza
shughuli za maendeleo.
Akizungumza kwa niaba
ya wananchi hao Ali
Hemedi alisema mwaka
2008 shirika la
bioshape lili kiomba kijiji
eneo la majaribio
ya kupanda miti ya aina ya
mibono baada ya kuwapa
walishindwa kuendelea na mradi kama ilivyokusudiwa
Hemedi alisema kushindwa
kuendelea kwa mradi
huyo ambao ulichukua hekta 16,000
umekifanya kijiji na wananchi
kukosa eneo la kuendesha shughuli za kilimo na kuwafanya
kuwa masikini kwa
kupatwa na njaa
kila mwaka.
Sophia Kilwanda alisema sambamba na Mwekezaji Bioshape
walitokea Wawekezaji Alhashumu
Company Ltd na Nitro Explossive Ltd
wamechukua hekta zaidi
ya 6000 ambazo wananchi wenyewe
hawakushirikishwa kikamilifu.
Sophia alisema kutokana kutoshirikishwa wanamuomba mkuu
wa mkoa kuwasaidia kwa hilo
hili Haki zao
waweze kuzipata.
Yusuphu Mohamedi
alisema migogoro ya ardhi wilayani humo
inasababishwa na watendaji wa idara ya
ardhi inayoongozwa na Hamidu
Mtemekela ambaye amekuwa chanzo cha
matatizo hayo.
Kwa upande wake
mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey
Zambi alisema ofisi yake
italishughulikia suala hilo na aliwataka
watendaji wa halmashauri
ya wilaya Kilwa akiwemo afisa
Ardhi kupeleka vielelezo
vinavyo husu migogoro hiyo.
Zambi alisema wilaya
kilwa inaongoza kwa kuwa
na migogoro ya ardhi
katika mkoa wa Lindi
hali ambayo hailete sura mzuri
na ana amini kuwa kuna kasoro
za kiutendaji ambazo
zanahitaji kurekebishwa.
Post a Comment